Wachezaji
na mashabiki wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya nchini Tanzania wakiwa
wamembeba mchezaji,Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa
Afrika wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) kwa kumfunga Vishen Jagdev wa
Afrika Kusini 6-4,katika mchezo uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa
wiki.
Wachezaji
na mashabiki wa timu ya Safari Pool kutoka Tanzania wakishandilia na
mchezaji Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa mchezaji mmoja
mmoja (Singles) Afrika uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji
wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya Tanzania wakiwa na medali zao za
Fedha mara baada ya kutunukiwa kwa kupata nafasi ya tatu katika
mashindano ya Pool Afrika yaliyofanyika jijini Blantyre Malawi mwishoni
mwa wiki.
Mgeni
rasmi,Mjumbe wa Baraza la Michezo Nchini Malawi, Sharaf Pinto(wa pili
kushoto) akiwa na mabingwa wa Singles(mchezaji mmoja mmoja).Kutoka kulia
ni mshindi wa tatu kutoka Zambia, Moses Mofya,mshindi wa pili kutoka
Afrika Kusini, Vishen Jagdev na Bingwa gwa Afrika kutoka Tanzania,
Patrick Nyangusi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwakabidhi
medali zao Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Mabingwa
wa Afrika wa mchezo wa pool wakiwa katika picha nya pamoja.Kutoka
kushoto ni Bingwa wa Afrika kutoka Tnzania, Patrick Nyangusi,mshindi wa
pili kutoka Afrika Kusini, Vishen Jagdev na mshindi wa tatu kutoka
Zambia, Moses Mofya mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao jijini Blantyre
Malawi mwishoni mwa wiki.
Bingwa
wa Afrika wa Safari Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi akiwa katika
picha ya pamoja na warembo wa Blantyre Malawi mara baada ya kukabidhiwa
zawadi ya medali ya zahabu mwishoni mwa wiki.


Post a Comment