KIJIJI cha Lulago, wilayani Kilindi mkoani Tanga, kimeingia
katika hofu kubwa baada ya mgambo Mbwana Salim kuuawa kutokana na kutoelewana
katika moja ya majukumu yake kikazi, huku askari polisi naye akipigwa risasi ya tumbo.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Costantine Masawe, pichani. Picha na Maktaba Yetu.
Baada ya kuuliwa kwa mgambo huyo na watu wasiofahamika, askari polisi waliingia na mmoja wapo kujikuta akipigwa risasi ya tumbo katika kadhia hiyo.
Baada ya kuuliwa kwa mgambo huyo na watu wasiofahamika, askari polisi waliingia na mmoja wapo kujikuta akipigwa risasi ya tumbo katika kadhia hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa za awali katika kijiji hicho, sakata
hilo lilianzia kwenye vurugu za wafanyabiashara ambao inasemekana waligoma
kulipa ushuru.
Kamanda wa Polisi Mkoa Tanga, Costantine Masawe,
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo wilayani Kilindi mkoani Tanga.
“Taarifa hizo zimetufikia kutokana na askari wetu kupigwa
risasi wakati anajaribu kutimiza majukumu yake na taarifa zaidi tutaendelea
kuzitoa juu ya tukio hilo,” alisema.
Kamanda Masawe alisema baada ya kutokea vurugu hizo na mgambo
kuuliwa, askari waliingia na kufukuzana na watu wanaosadikiwa kuwa walishiriki
kwenye tukio hilo, ambapo mwisho wake ulifikia kwa askari kupigwa risasi ya
tumbo na sasa yupo hospitali akipatiwa matibabu.
Post a Comment