MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amewataka
wadau mbalimbali kuacha kulichukulia kisiasa suala la ruzuku badala yake
taratibu na sheria zifuatwe. Akizungumza na RAI ofisini kwake jijini
Dar es Salaam jana, Jaji Mutungi alisema ingawa jambo hilo linahusisha
vyama vya siasa, ukweli ni kwamba limebeba maslahi ya taifa, hivyo si
vyema kuchukuliwa kisiasa zaidi.
“Haya si masuala ya kukurupuka na ndiyo maana hata katika ziara nilizofanya kwenye ofisi za vyama baada ya kuteuliwa kushika nafasi hii nilisisitiza kuwa Ofisi ya Msajili iko wazi na inafanya shughuli zake kwa umakini mkubwa. Yapo masuala ya kisiasa yanayopaswa kubebwa hivyo lakini mengine ni lazima taratibu na sheria zifuatwe,” alisema Jaji huyo aliyepokea ofisi kutoka kwa Jaji John Tendwa miezi michache iliyopita.
Alisema ofisi hiyo itajiridhisha kwanza kabla ya kuchukua hatua kuhusu mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ya kusitishwa utoaji wa ruzuku kwa vyama vyote vya siasa nchini, hadi hesabu zao zitakapokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
“Hakuna kukurupuka. Tunajiridhisha kwanza kwa kuzingatia vigezo vilivyoelekezwa kisheria kwani ni hivyo ndivyo vitatuweaesha kusitisha ruzuku kwa vyama. Kutohusisha sura ya siasa hakuondoi umuhimu wa wanachi kupata taarifa sahihi kuwa fedha zao zinatumika vipi,” alisema.
Jaji Mutungi alionekana kushangazwa na mvutano ulioibuka akisema kuwa suala la ukaguzi haliepukiki na kwamba kila idara inapaswa kutekeleza wajibu wake.
“Kama suala ni sheria, basi ifanyiwe marekebisho kwani kila upande una haki. PAC wana haki na vyama pia vina haki kutolewa taarifa zilizo sahihi. Sasa mvutano unatoka wapi? Hili si suala la ushabiki kama wa Simba na Yanga,” alisema
Hivi karibuni Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe, iliagiza kusitishwa mara moja utoaji wa ruzuku kwa vyama vyote vya siasa nchini hadi hesabu zake zitakapokaguliwa naCAG, agizo lililozua mjadala ndani ya vyama vya siasa na miongon mwa Watanzania.
Akitoa uamuzi wa kamati hiyo ya Bunge jijini Dar es Salaam, Zitto alisema tangu mwaka 2009 vyama vyote vya siasa vinavyopata ruzuku ya Serikali havijawahi kupeleka ripoti yoyote ya ukaguzi wa fedha kwa CAG, huku vikiwa vimepokea ruzuku ya jumla ya Sh bilioni 67.7 kwa vyama tisa vya siasa.
Alivitaja vyama hivyo kuwa ni pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho kimekwishapokea ruzuku ya Sh bilioni 50.9, Chadema Sh bilioni 9.2 na Chama cha Wananchi (CUF) Sh bilioni 6.3.
Vyama vingine ni NCCR-Mageuzi Sh milioni 677, UDP Sh milioni 333, TLP Sh milioni 217, APPT Maendeleo Sh milioni 11, DP Sh milioni 3.3 na CHAUSTA Sh milioni 2.4.
RAI

Post a Comment