Na Mwandishi Wetu,Arusha
Mkutano wa kwanza katika historia
ya Chama cha Kimataifa cha Taasisi za Kitaifa cha afya za
Jamii(IANPHI),umefungwa jana jioni na kuwapa fursa wageni hao kutoka
nchi 35 ulimwenguni kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kujionea
vivutio mbalimbali.
Mkutano huo ulianza Septemba 29
hadi Oktoba 1,2013 katika hoteli ya kitalii ya Ngurdoto huku mada
mbalimbali zikitolewa na kuwapa uelewa mkubwa washiriki.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo,Dk Mwele Malecela amesema mkutano huo umekuwa na mafanikio
makubwa kutokana na umuhimu wa taasisi za afya ya jamii katika mataifa
mbalimbali.Ambao umejadili namna ya kukabiliana na magonjwa yaliyokuwa
hayapewi kipaumbele na magonjwa yanayoambukizwa kutokomezwa.
"Tumejadili kwa kina kuhusu
magonjwa yasiyoambukizwa ambayo ni tatizo kubwa katika mataifa mengi
hasa Afrika na kuona wenzetu wamefanikiwa kwa kiwango gani kukabiliana
nayo,tumepata uzoefu kutoka kwa wataalamu wa Mexico ambao wameonesha
wasiwasi wao juu ya matumizi ya vinywaji vyenye sukari ambavyo
vinapatika kwa urahisi sana hapa nchini kuwa ni jambo la hatari,
Pia tumezungumzi umuhimu wa
taasisi hizi baada mwaka 2015 ziangalie namna kujipanga mambo kwa mapana
zaidi katika kutokomeza magonjwa yaliyoanishwa,"amesema Dk Mwele.
Katika hatua nyingine Dk Mwele amechaguliwa kuwa Rais wa muda wa Chama
cha Kimataifa cha Taasisi za Kitaifa cha afya za Jamii(IANPHI) Chapter
ya Afrika ili kuwa na sauti moja katika mikutano ya kimataifa.
Mkutano wa taasisi hizo wa mwaka 2014 utafanyika katika nchi ya Morocco
Post a Comment