Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA YAENDESHA MAFUNZO KWA MAKATIBU TAWALA NA WAKURUGENZI


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma , George  Yambesi akifungua mafunzo kwa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara .
 Sehemu ya washiriki wa mafunzo wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  George  Yambesi.
Mmoja kati ya washiriki, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimajanro Dk. Faisal Issa akizungumza kuhusu mafunzo hayo, na kutoa shukrani.
Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wametakiwa kuhakikisha matatizo ya mishahara kwa watumishi yanamalizika mara moja

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuhusu Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na  Mishahara (HCMIS). Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Mejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi alisema  malalamiko ya watumishi kuhusu malipo ya stahili zao kwa wakati yamepungua, pia kudhibiti eneo la mikopo kwa watumishi kwa kuhakikisha makato kwa ajili ya mikopo hiyo hayavuki theluthi mbili za mishahara yao.
“Mtakua mmetoa mchango mkubwa katika eneo hili kama kila mtumishi atakuwa na taarifa sahihi kwa kutumia mfumo huu ili taarifa hizo ziweze kutumiwa kufanya maamuzi sahihi katika eneo la usimamizi na matumizi bora ya watumishi” Ka Yambesi alisema na kuongeza mafunzo hayo yamelenga ufahamu wa mfumo, mahitaji maalum kwa uendeshaji na usimamizi katika ngazi ya waajiri.
 Mafunzo hayo yalikuwa mahususi kwa Makatibu Tawala na wakurugenzi
Yambesi aliainisha kuwa lengo la mafunzo hayo ni kutekeleza au kufanya maamuzi ya kiutumishi kwa weledi unaotakiwa na kwa kufanya hivyo washiriki hao wa mafunzo watakuwa wameshiriki kutoa mchango wao katika mabadiliko yanayoendelea kwa maendeleo na ustawi wa Taifa kupitia huduma mbalimbali zinazotolewa.
Katibu Mkuu aliwaelekeza baada ya kuelewa mfumo wa HCMIS unavyofanya kazi na taarifa muhimu zinazoweza kutolewa na mfumo huo watafakari namna ya kuufikisha mfumo huo katika maeneo yao ya huduma mfano katika sekta za Elimu, Afya, Kilimo na Mifugo.
Yambesi aliongeza pia ni vizuri kutafakari namna mfumo huo utakavyoweza kutumika kuimarisha usimamizi katika maeneo mengine ya malipo ya stahili za watumishi kama vile madai ya likizo, matibabu na mafunzo ambayo yanaendelea kukua bila udhibiti wa kutosha hivyo mfumo kutumika kupata sulushisho kwa madai mengi ya watumishi yanayojitokeza.
Kwa kutumia mfumo huu mtaweza kufanya maamuzi mbalimbali na kusimamia watumishi walio chini yenu kwa kuimarisha uwajibikaji na kupunguza muda mwingi mliokuwa mnatumia kupata taarifa za kiutumishi kwa ajili ya kufanya maamuzi, pia kuwa na taarifa sahihi na kwa wakati kuhusiana na utekelezaji wa maagizo mnayotoa.
Mfumo wa HCMIS ulianzishwa mwaka 2010 ukiwa na lengo la kuimarisha usimamizi wa rasilimaliwatu na mishahara katika utumishi wa Umma kwa kuhakikisha watumishi wanaingizwa kwenye orodha ya malipo ya mishara (Payroll) kwa wakati, mishahara na cheo cha mtumishi kinabadilishwa kwa wakati anapopandishwa cheo, kuepuka malimbikizo makubwa ya muda mrefu ya mishahara ya watumishi, watumishi wanaondolewa kwenye orodha ya malipo kwa wakati, na pia serikali inakuwa na taarifa sahihi za watumishi na kuzitumia kufanya mipangilio ya rasilimali na mishahara.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top