Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

‘Msirudie makosa kuchagua viongozi wenye mapepo’

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT), Sophia Simba, amewataka wakazi wa Jiji la Mbeya, kutorudia makosa ya kuchagua viongozi walioghubikwa na ‘mapepo’ kuwakilisha matatizo yao bungeni. Kauli hiyo aliitoa mjini hapa juzi katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia UWT Mkoa wa Mbeya.

Sophia ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto alisema wana Mbeya wamefanya kosa moja kubwa la kuchagua viongozi ambao ni wawakilishi wa matatizo yao bungeni walioghubikwa na mapepo, vitendo vya kihuni na kibabe.

“Wana Mbeya acheni kutuletea mapepo bungeni, maana kwa sasa mmeleta pepo,” alisema Sophia.

Alisema kiongozi anapaswa kuonyesha mfano bora na si uhuni wa kutumia ubabe na kufanya vurugu katika jengo ambalo kila mtu anayeingia ni lazima afuate sheria na taratibu zilizopo.

“Bungeni kuna taratibu na sheria zake na watu wanaoingia ni lazima wazifuate kanuni hizo si kwa uhuni au ubabe kama wengine wanavyofikiria,” alisema Sophia.



Alisema kiongozi bora ni yule atakayetekeleza kwa vitendo baadhi ya ahadi alizozitoa kwa wapiga kura wake ikiwa ni pamoja na kusimamia na kuhakikisha miradi ya maendeleo inawafikia wananchi ambao ni walengwa na si kuhamasisha vurugu ambazo zimekuwa ni moja ya changamoto zinazorudisha maendeleo nyuma.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Baraza la CCM Taifa, Chazi Mwakipesile, alimtaka Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), kutekeleza ahadi alizozitoa kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na ile ya kuchimba mabwawa ya samaki kila kata.

“Ningemshauri rafiki yangu Sugu ni vema akajikita zaidi kutekeleza ahadi alizozitoa kwa wananchi wake za kuchimba mabwawa ya samaki kila kata, kuliko kuendelea na vitendo vya kitoto ambavyo vimekuwa vikirudisha nyuma maendeleo,” alisema Mwakipesile.

Aliwataka wakazi wa Mbeya hususani vijana, kubadilika na kuondokana na fikra au mtazamo wa kwamba kuzomea viongozi wa kitaifa ndio suluhisho ya matatizo yao.

“Mbeya tuna picha si nzuri kwa wageni na wawekezaji wetu ambao wamekuwa wakiogopa kuwekeza kutokana na kushamiri kwa vitendo vya vurugu zinazofanywa na watu wachache ambao wengi wao hawafahamu nini maana ya maendeleo,” alisema Mwakipesile.

MTANZANIA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top