Na. Aron Msigwa -MAELEZO.
Serikali
imetoa wito kwa wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kuendelea
kuwekeza katika sekta ya michezo , kuibua na kuendeleza vipaji vya
vijana walio katika maeneo mbalimbali nchini.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabrile ametoa wito huo leo jijini Dar es salaam wakati wa
Bonanza la mchezo wa mpira wa miguu lililowahusisha vijana kutoka
katika vituo 9 vya kulelea watoto walio katika mazingira magumu na
shule zilizo jirani na vituo hivyo jijini Dar es salaam.
Prof.
Elisante ameeleza kuwa Tanzania kwa sasa ina fursa nyingi za uwekezaji
katika sekta ya michezo na kuongeza kuwa serikali kwa kuliona hilo
inaendelea kuwezesha na kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha
kuwa sekta hiyo inapiga hatua kutokana na mchango wake katika katika
kudumisha amani na upendo, kukuza ajira ,uzalendo na ushirikiano.
“Sekta
ya michezo nchini sasa inapiga hatua kwa kuwahamasisha vijana wengi
kushiriki katika mashindano mbalimbali na kutumia fursa zilizopo
kujiajiri na serikali tutaendelea kutoa msukumo kwa wadau mbalimbali
kuingia katika juhudi hizi za kusaidia vikundi mbalimbali vya michezo
vilivyopo nchini” amesema Prof. Elisante.
Kuhusu
Bonanza la mchezo wa mpira wa miguu kwa vijana wanaoishi katika vituo
vya kulelea watoto walio katika mazingira magumu lililofanyika leo
jijini Dar es salaam amesema wengi wa vijana hao walikua wamekata tama
kutokana na wengi wao kukosa wazazi kutokana na sababu moja au nyingine
na kuwataka vijana hao ambao wengi sasa wamefanikiwa kuendelea na
masomo yao katika ngazi mbalimbali kuzitumia fursa walizopata ili
kutowakatisha tama wafadhiri.
Amewataka
vijana waliofanikiwa na kupiga hatua kimasomokuwasai dia wenzao ambao
bado wanahitaji msaada walio ndani ya vituo hivyo na wale ambao bado
wako mitaani.
Kwa
upande wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Diana Melrose
ameeleza kuwa kufanyika kwa bonanza hilo jijini Dar es salaam ni ishara
kubwa ambayo imeonyesha kuwa vijana wengi walio katika mazingira magumu
wakipewa fursa wanafanya mambo makubwa.
Amewapongeza
vijana hao kwa kuonyesha mfano wa kushiriki katika bonanza la
mashindano hayo ambapo washindi pamoja na mambo mengine wamekabidhiwa
medali huku kombe likienda kwa timu ya mpira wa miguu ya kituo cha
dogodogo cha jijini Dar es salaam.
Naye
mratibu wa mashindano hayo kutoka “British Council” Bi. Malula
Nkanyemka ameeleza kuwa lengo la kuanzishwa kwa mashindano hayo mbali na
kuibua vipaji na kuwajengea uwezo vijana hao kimichezo yanalenga
kuwafanya vijana hao kujitambua na kuzitumia haki zao, kucheza na
kubadilisha tabia.
Mashindano
hayo yaliyoratibiwa kwa ushirikiano na Ubalozi wa Uingereza nchini
Tanzania, British Council, Rotary Club, Baraza la Michezo Tanzania
(BMT), Right lo Play, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na
wenyeji wa bonanza hilo shule ya sekondari Kibasila yamefanyika katika
viwanja vya michezo vya shule ya sekondari Kibasila na kuzishirikisha nyumba 9 za kulelea watoto walio katika mazingira magumu na.
Post a Comment