Ofisi ya Inspekta
Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734 Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556 S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja: DAR ES SALAAM.

02/10/2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania inatarajia kupokea Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri kwa Nchi za maziwa makuu na pembe ya Afrika katika mapambano ya kuzuia na kudhibiti uzagaaji wa silaha haramu (RECSA) kutoka nchi ya Rwanda.
Makabidhiano hayo yatafanyika kesho tarehe 03/10/2013 katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ya Rwanda atamkabidhi uenyekiti huo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Tanzania Mh.Dk Emmanuel Nchimbi.
Uenyekiti huo utadumu kwa muda wa miaka miwili ambapo katika kipindi hicho mikutano yote ya kukabiliana na uzagaaji wa silaha haramu itaratibiwa na Nchi ya Tanzania kupitia Jeshi la Polisi.
Umoja huo ulianzishwa mwaka 2005 kwa madhumuni ya kudhibiti uzagaaji wa silaha haramu kwa nchi za maziwa makuu na pembe ya Afrika ambazo ni pamoja na Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania.

Imetolewa na
Advera Senso – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi(T)
Advera Senso – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi(T)
Post a Comment