Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
*******
Serikali
ya Tanzania imesema inatafakari ushiriki wake ndani ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki na inaweza kujitoa ndani ya Jumuiya hiyo iwapo
itaendelea kutengwa katika baadhi ya vikao.
Aidha
imesema Tanzania haitambui vikao vinavyofanywa na nchi tatu zilizopo
ndani ya Jumuiya hiyo ambazo zimekuwa zikizitenga Tanzania na Burundi.
Waziri
anayehusika na masuala ya Afrika Mashariki wa Tanzania Samwel Sitta
ameliambia Bunge la Tanzania kuwa makubaliano ya vikao hivyo
vinavyofanywa na nchi za Kenya, Rwanda na Uganda yatatekelezwa na nchi
hizo zinazofanya vikao hivyo kwa sababu vinafanyika nje ya utaratibu wa
mkataba wa jumuiya hiyo.
Katika mikutano iliyofanyika hivi karibuni Tanzania na Burundi hazikualikwa kwenye vikao hivyo.
Kwa
mujibu wa Waziri Sitta mikutano ya wakuu wa nchi za Rwanda, Kenya na
Uganda ambayo ilianza kwa kuitenga Tanzania ilifanyika Entebbe nchini
Uganda mwezi Juni mwaka huu na kufuatiwa na mkutano wa pili uliofanyika
Agosti mwaka huu huko Mombasa nchini Kenya ambapo nchi hizo tatu bila
kuishirikisha Tanzania walizungumzia uanzishaji wa himaya moja ya
forodha.
Mambo
mengine waliyozungumza wakuu hao ilikuwa uanzishaji wa visa moja ya
utalii kwa nchi zao na matumizi ya vitambulisho vya uraia ambavyo
vitatumika kama hati za kusafiria miongoni mwa nchi hizo.
Aidha Waziri Sitta amesema ndani ya mikutano hiyo pia walizungumzia kuanzisha mchakato wa kuanzisha shirikisho la nchi hizo.
Tayari
Tanzania imeanza mazungumzo na nchi za Burundi na Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo kuangalia ni kwa namna gani zitaanzisha ushirikiano
nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama zinavyofanya nchi za Rwanda,
Uganda na Kenya. Source: BBC Swahili
Post a Comment