Pichani
juu na chini ni Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule za msingi
za Zanaki, Diamond, Kisutu na Muhimbili katika siku maalum
inayotambulika kama “Fun Thursday” na kufanyika Alhamis ya mwisho wa
mwezi.
Bi.
Ledama ametumia siku hiyo kuwaelimisha wanafunzi kuhusiana na kazi
mbalimbali zinazofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini yakiwemo
Malengo ya Milenia ambayo ni Kutokomeza umaskini uliokithiri na njaa,
Elimu ya Msingi kwa wote, Usawa wa kijinsia na fursa sawa kwa wanawake,
kupunguza vifo vya watoto wachanga, Upatikanaji wa huduma bora za uzazi,
kupambana na Ukimwi, Malaria na magonjwa mengine, kulinda mazingira
pamoja na kujenga mshikamano wa kimaendeleo duniani. Fun Thursday imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za UNESCO jijini Dar leo.
Wanafunzi
wakimsiliza kwa umakini wakati Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani) wakati
akiwapiga msasa kuhusiana na kazi mbalimbali zinazofanywa na mashirika
ya Umoja wa Mataifa nchini.
Msaidizi
wa Maktaba ya kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi.
Harriet Macha akiwaelezea wanafunzi umuhimu wa kuwa na Maktaba mashuleni
mwao pamoja na kujijengea tabia za kupenda kujisomea.
Wanafunzi
wakifurahi wakati wa Fun Thursday inayofanyika kila Alhamis ya mwisho
wa mwezi na kuratibiwa na Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC).
Mwalimu
Nicholaus Massawe wa shule ya msingi Zanaki akibadilishana mawazo na
Mwalimu Rahel Fute wa Shule ya msingi Diamond wakati wa Fun Thursday
iliyowakutanisha wanafunzi kutoka shule za msingi mbalimbali za jijini
Dar.
Mratibu
wa Mkoa kutoka Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) Innocent
Mkota akiwasisitiza wanafunzi umuhimu wa kujiunga na vilabu vya Umoja
wa Mataifa mashuleni.
Wanafunzi
wa shule za mbalimbali za msingi jijini Dar es Salaam wakifuatilia
Documentary fupi iliyomshirkisha msaani wa muziki wa Marekani Beyonce na
wimbo wake wa “I was here” inayoenyesha kazi mbalimbali zinazofanywa na
mashirika ya Umoja wa Mataifa Duniani.
Mwalimu
Kalabo Mushumbusi kutoka shule ya Msingi Muhimbili akitoa shukrani kwa
kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC kuwa kuwaelimisha wanafunzi
wao kuhusiana na kazi mbalimbali ya Umoja Mataifa nchini.
Wanafunzi
wa shule za msingi jijini Dar wakiwa kwenye picha ya pamoja na
wafanyakazi wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) pamoja na
walimu wao nje ya ukumbi wa mikutano wa Ofisi za UNESCO.
Post a Comment