Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Dkt. Anselm Tarimo.
Serikali
Mkoani Shinyanga imetoa rai kwa watendaji wote hususani Wakurugenzi wa
Mamlaka za serikali za mitaa kusimamia kazi za barabara kwa kufuata
sheria na kanuni kinyume chake serikali haitasita kuchukua hatua kwa
watendaji ambao watashindwa kusimamia miradi kwa umakini.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga ametoa rai hiyo jana kwenye
kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mhe.Rufunga
amesema,usimamizi mbovu unaisababishia serikali gharama za matengenezo
zisizo za lazima,hivyo kuathiri shughuli za miradi mingine ya maendeleo
pamoja na kuhatarisha usalama wa watumiaji wa barabara.
Amesisitiza
watendaji kutumia wakandarasi wanaostahili kielimu na vifaa vya
kutosha, kuepuka rushwa na Wakurugenzi wote na Katibu Tawala
Mkoa,kufanya ukaguzi wa barabara ili kujiridhisha utekelezaji wake.
Amesema
pia,wananchi wote wana jukumu la kuzilinda barabara na kuzitunza kwani
ni muhimu katika shughuli za maendeleo kwa kusafirisha bidhaa mbalimbali
na kushirikiana kuwabaini wanaohujumu miunndombinu hiyo ili wafikishwe
kwenye vyombo vya sheria.
Aidha,Mkuu
wa Mkoa amemtaka Wakala wa barabara wa Mkoa kuwaelimisha watumiaji wa
barabara matumizi ya alama mbalimbali za barabara na kufanyia
matengenezo alama zilizoharibiwa.
Katika
kikao hicho wajumbe wameazimia Mkoa uandae Kamusi ya mtandao wa
Barabara unaoonesha barabara zote katika Mkoa wa Shinyanga wenye urefu
wa Kilometa 5,126.22.
Vilevile
mkoa unatarajia kujenga barabara moja yenye manufaa kiuchumi
inayounganisha Mkoa wa Shinyanga na Mkoa wa Mwanza kupitia Halmashauri
za Manispaa ya Shinyanga,Wilaya ya Shinyanga na Halmashauri ya Mji
Kahama na Halmashauri ya wilaya ya Msalala ambapo upembuzi yakinifu
umeshafanyika na itagharimu jumla ya Tshs.Bilioni 118.
Hoja
nyingine muhimu iliyojadiliwa na wajumbe wa kikao hicho ni uzito wa
mizigo ambao hauendani na uwezo wa barabara, ambapo wajumbe wametaka
alama zinazoonesha uwezo wa barabara ili kudhibiti uzito wa mizigo
inayozidi na inayoletea uharibifu wa barabara.
Meneja
wa Wakala wa barabara Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Philipo Manenuka
amesema sheria ya kuweka alama za kuonesha uzito wa barabara inatamka
kuwa ni mamlaka yenyewe ya serikali za mitaa ndiyo inaamua.
Post a Comment