Baadhi
ya washiriki wa warsha ya pamoja kwa wadau wa sekta ya nishati
wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi
(hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa saba uliofanyika leo
katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam. Serikali
imekamilisha utafiti katika vituo 52 vya kutoa umeme wa joto ardhi
(geothermal) na ifikapo mwakani uchimbaji wa umeme huo utaanza katika
vituo vitatu vilivyopo katika mkoa wa Mbeya, wilaya ya Rufiji na katika
ziwa Natroni lililo mkoani Manyara.
Katibu
Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi (kulia)
akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Ngosi Mwihava
(katikati) wakati wa warsha ya pamoja ya siku moja kwa wadau wa sekta ya
nishati iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishina wa masuala ya Nishati na Mafuta
Eng. Hosea Mbise.
Katibu
Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi (kulia) akifuatilia
mada iliyokuwa inawasilishwa na Dk. Lennart Larsson wakati wa warsha ya
pamoja ya siku moja kwa wadau wa sekta ya nishati iliyofanyika leo
katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Kamishina wa masuala ya Nishati na Mafuta Eng. Hosea Mbise.
Katibu
Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi (kushoto) akiongea
na Dk. Lennart Larsson (kulia) mara baada ya ufunguzi wa farsha ya
pamoja ya siku moja kwa wadau wa sekta ya nishati iliyofanyika leo
katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi akifungua warsha ya
pamoja kwa wadau wa sekta ya nishati leo katika Hoteli ya Hyatt
Regency iliyopo jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo wa saba
uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency mambo mbalimbali
yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na masuala ya mafuta, umeme na gesi.
Katibu
Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi (kulia) akiongea
jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Ngosi Mwihava wakati wa
warsha ya pamoja kwa wadau wa sekta ya nishati iliyofanyika leo katika
Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Serikali imekamilisha
utafiti katika vituo 52 vya kutoa umeme wa joto ardhi (geothermal) na
ifikapo mwakani uchimbaji wa umeme huo utaanza katika vituo vitatu
vilivyopo katika mkoa wa Mbeya, wilaya ya Rufiji na katika ziwa Natroni
lililo mkoani Manyara.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Post a Comment