Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina Madete akifungua warsha ya siku mbili kwa wafanyakazi kutoka
sekta mabalimbali za Serikali juu ya mafunzo kuhusu kuenea kwa Hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya
ardhi mjini Bagamoyo leo.
sekta mabalimbali za Serikali juu ya mafunzo kuhusu kuenea kwa Hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya
ardhi mjini Bagamoyo leo.
Sehemu
ya wajumbe wa warsha ya mafunzo kuhusu kuenea kwa hali ya jangwa na
ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini Bagamoyo wakiskliza hotuba
iliyokuwa ikitolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia
Angelina Madete. Wajumbe wa warsha ya mafunzo kuhusu kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini
Bagamoyo leo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi katika warsha hiyo Injinia Angelina Madete.
Bagamoyo leo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi katika warsha hiyo Injinia Angelina Madete.
…………………………………………………………………….
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina Madete amesema
ukame umekuwa tatizo kubwa sana katika nchi zinazoendelea ikiwamo
Tanzania. Na pia umeleta athari sana katika swala zima la mazingira,
ameongeza kuwa katika Africa inakadiriwa aslimia 73 ya nchi imepunguza
uwezo wa kuzalisha chakula na hii imepelekea kuongezeka kwa ukame na
hivyo kupelekea upungufu wa chakula Nchini. Alitaja baadhi ya mikoa
iliyoathiriwa na ukame ambayo ni Dodoma, Singida na maeneo machache ya
mikoa ya Shinyanga,Mara, Iringa, Manyara na Arusha.
Amesema
hayo leo mjini Bagamoyo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili
kuhusu juu ya kuenea kwa hali ya jangwa na ukame wa maendeleo
endelevu ya ardhi. Warsha hiyo imewashhirikisha wafanyakazi kutoka
wizara mbalimbali za Serikali kwa lengo la kuwaongezea uelewa juu ya
umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa lengo kuepuka janga la ukame..
Akiongea
katika warsha hiyo Injinia Madete alisema kuwa ukame unaleta umaskini
na pia ukame umechangia wananchi wengi kuhama maeneo yao na kwenda
sehemu zingine zisizo na ukame. Aliendelea kusema kuwa Serikali
imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na swala hilo la ukame amabapo
mwaka 1994 ilisaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupamabana na kuenea
kwa hali ya jangwa na ukame(United Nations Convetion to Combat
Dessertification UNCCD) na pia serikali inatekeleza mkataba huo kupitia
Programu ya Taifa ya kupambana na kuenea kwa hali ya Jangwa na
ukame(Nationala Action Programme to Combat Dessertification-NAP). Na
kususdi kubwa la mkataba huu ni kuimarisha maisha ya kila siku ya
mwananchi wa kawaida aishiye kwenye sehemu za Ukame.
Warsha
hiyo ya siku mbili imewashirikisha pia wadau wa mazingira kutoka sehemu
mbalimbali wakiwemo wafadhili kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja Wa
Mataifa (UNDP)
Post a Comment