Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Taswira ya Ziara ya rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Makete mkoa wa Njombe

 


fr13
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoka kuweka jiwe la msingi madarasa ya kidato cha tano shule ya sekondari lupalilo.
fr19
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiongea na Bi Sarah Mageni Sanga, mlemavu ambaye Rais alimpa pikipiki ya Bajaji pamoja na mtaji wa pesa taslimu wa shilingi milioni mbili October 28, 2009 baada ya kuguswa na mkasa wa maisha ya mkaazi huyo wa kijiji cha Lupalilo wilaya ya Makete mkoa wa Njombe alipomuona akohojiwa katika TV na kueleza kuwa maisha yake ni magumu mno baada ya ndugu na jamaa zake wote kuteketea kwa maradhi ikiwa ni pamoja na UKIMWI. Pichani Bi Sanga akimshukur Rais kwa msaada huo ambao amesema umebadili kabisa maisha yake kwani sasa anaishi kama mtu yeyote kijijini hapo
  fr23
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wananchi wa kijiji cha Ivalalila wilayani Makete baada ya kuweka jiwe la msingi la kituo cha afya cha kijiji hicho mwishoni mwa juma. fr27
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi  Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA cha Wilaya ya Makete mwishoni mwa juma
fr28
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia ubora wa shati lililotengenezwa na wanafunzio wa Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA cha Wilaya ya Makete baada ya kukifungua rasmi chuo hicho mwishoni mwa juma.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top