Msemaji toka Wizara ya Kazi na Ajira Bw.Ridhiwan Wema(Kulia) akieleza
kwa waandishi wa habari kuhusu majukumu ya Bodi za Mishahara Kisekta kwa
mujibu wa sheria Na. 7 ya Mwaka 2004 ya Taasisi za Kazi katika Sekta
Binafsi, wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya
Habari(MAELEZO) Leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mchumi Mwandamizi
wa Wizara hiyo Bw. Jofrey Mashafi.
Afisa
Kazi Mwandamizi toka Wizara ya Kazi na Ajira(kulia) akieleza kwa
waandishi wa habari(Hawapo pichani) jinsi ukuaji wa sekta unavyochangia
kuanzishwa kwa bodi ya Mshahara kwa Sekta husika wakati wa Mkutano
uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo jijini Dar es
Salaam. Msemaji Wizara hiyo Bw.Ridhiwan Wema. Mchumi
Mwandamizi toka Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Jofrey Mashafi (kulia)
akieleza mipango ya serikali ya kukabiliana na tatizo la upungufu wa
Ajira Nchini ikiwa ni pamoja kuanzisha programu ya miaka 3 inayoratibiwa
na Wizara ya Kazi na Ajira kwa kushirikiana Chuo cha Sokoine na Bank
ya CRDB ya kuwajengea uwezo wahitimu wa vyuo vikuu, inayotarajiwa
kuzalisha ajira 30,000, wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa
Idara ya Habari (MAELEZO) Leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa
Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Georgina Misama.
Picha na Frank Mvungi-MAELEZO
…………………………………………………………………………………
WIZARA ya Kazi na Ajira imewaasa waajiri katika Sekta binafsi kuzingatia Sera na sheria za kazi mahali pa kazi ili kuleta tija na nidhamu kazini.
Hayo
yamesemwa na Msemaji wa Wizara hiyo Ridhiwani Wema wakati wa mkutano na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, akieleza kuhusu utaratibu
wa uanzishwaji wa Bodi za mishahara kisekta ili kusaidia kuboresha
maslahi ya wafanyakazi.
Wema
amevishauri vyama vya wafanyakazi kuboresha mishahara na maslahi ya
wafanyakazi kupitia majadiliano ya pamoja sehemu za kazi kwa kuwa
sheria na kanuni zinatoa na kuhimiza haki hizo.
Alizitaja
bodi za mishahara zilizoanzishwa kuwa ni kilimo, Afya, Biashara na
Viwanda, Mawasiliano, Madini, Uvuvi na huduma za majini, hoteli na
huduma za majumbani, na ulinzi binafsi.
Wema
alifafanua kuwa katika kipindi cha mwaka 2011 hadi sasa ziliundwa bodi 4
za mishahara kufanya jumla ya bodi za kisekta kuwa 12 hadi mwaka 2013.
“Moja
ya majukumu ya bodi ni kufanya uchunguzi kuhusu kima cha chini cha
mishahara na hali ya ajira katika sekta husika ambapo pia humshauri
Mhe. Waziri kuhusu kima cha chini cha mishahara pamoja na masharti ya
ajira katika sekta husika”, alisema Wema.
Alibainisha
kuwa Bodi za ajira zimetembelea mikoa ya Daressalaam, Mororogoro,
Pwani, Dodoma, Arusha, Mwanza, Tanga, Manyara, Iringa, Mbeya na
Kilimanjaro ili kijionea mazingira ya kazi na kupata maoni ya wadau
kuhusu kima cha chini cha mishahara katika Sekta husika.
Msemaji
huyo aliongeza kuwa vyama vya wafanyakazi vina nafasi kubwa kusaidia
katika kuboreshwa kwa maslahi ya wafanyakazi kupitia majadiliano ya
pamoja sehemu za kazi kwa kwa kuwa sheria na kanuni zinatoa na kuhimiza
haki hiyo.
Naye
Afisa Kazi Mwandamizi Idara ya Ajira, Ayubu Musa alisema kuwa wizara
hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa taratibu, sheria na
kanuni za kazi zinazingatiwa ambapo wamekuwa wakifanya ukaguzi mara kwa
mara ili kuhakisha kuwa kuna mazingira bora na maslahi ya wafanyakazi
katika sekta binafsi.
Bodi
za mishahara kisekta zinaundwa kwa mujibu wa sheria ya Taasisi za kazi
namba 7 ya mwaka 2004 ambapo kila bodi inaundwa na wajumbwe 8 akiwemo
mwenyekiti na wajumbe wanaowakilisha maslahi ya Serikali wajumbe
2,waajiri wajumbe2 na wafanyakazi 2 katika mfumo wa utatu.
Post a Comment