…………………………………………………
Vijana hapa nchini wametakiwa
kuacha kukaa vijiweni na kulaumu serikali wakati hawatumii fursa
mbalimbali ikiwemo fursa ya ujasiriamali na fursa nyinginezo kwa manufaa
ya maisha yao ya baadae.
Kauli hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wizara ya habari
vijana utamaduni na michezo Elisante Ole Gabriel wakati alipokuwa
akifungua maonyesho ya ujasiriamali kwa wahitimu wa stahahada ya uzamili
wa masuala ya ujasiriamali kwenye chuo cha ESAMI kilichopo jijini hapa.
Ole Gabriel alisema kuwa
serekali imetenga jumla y ash 6.1 bilion kwa ajili ya kuwawezesha vijana
watakao ibua miradi mbalimbali kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa
ujumla na kuwataka vjana kutumia fursa hizo kwa manufaa yao ya baadae
ilikutimiza ndoto zao.
‘’Hapa mmejionea ndoto mbali
mbali za vijana hawa ambao wakitoka hapa teyari ni wajasiriamali wakubwa
kwani maonyesho kama haya yanakuza vijana kuweza kujiajiri na
kuondokana na fikra za kuajiriwa na viomba vyuo mbali mbali hapa nchini
kuanza kuiga mfano wa chu hiki cha ESAMI kwani haya ndiyo mawazo
serekali inayataka’’alisema ole Gabriel.
Nae Makamu mkuu wa chuo hicho
Joseph Mumba alisema kuwa vyou na taasisi kwenye nchi nyingi za Afrika
vimekuwa vikianda vijana kuingia kwenye soko la kuajiriwa na kuacha
kuwapatia uwezo vijana wetu kuweza kujiajiri hapa maendeleo yetu
yatabaki kuwa yakusuasua na hakuna wakumlaumu kwenye hili.
Mumba pia alisema ukipita
mitaani utakutana na vijana wakiwa kwenye maeneo mbalimbali bila ya
ajira huku wakiwa na uwezo na elimu ya kutosha hapa tatizo ni maandalizi
ya vijana hawa kuwapa elimu ya kuwawezesha kujiajiri.
Aidha mkurugenzi wa kitengo
hicho cha ujasiriamali chuoni hapo Leon Malisa alisema kuwa maonyesho
hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza chuoni hapo na kuwa wengi wa
wanafunzi wa stahada ya uzamili ngio wanaoonyesha maonyesho hayo kwa
vitendo jinsi walivyoyapokea mafunzo yao.
Malisa alisema kuwa mafunzo ya
ujasiriamali ya maonyesho yatakuwa yakifanyika kila mwaka kwa wanafunzi
kuonyesha jinsi walivyoyapokea mafunzo hayo.
Post a Comment