Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel akitoa somo kwa vijana kutoka maeneo mbalimbali
nchini kuhusu namna wanavyoweza kutumia fursa zilizopo kupambana na
umasikini na tatizo la ajira wakati wa mdahalo wa Wiki ya Vijana leo
mkoani Iringa.(PICHA NA ARON MSIGWA-IRINGA)
Picha ya pamoja
…………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa Iringa.
Vijana
kote nchini wametakiwa kuacha tabia ya kulalamika na badala yake
wazitumie fursa za kiuchumi zilizopo katika maeneo yao kubuni miradi
mbalimbali na kufanya kazi kwa bidii ili jamii iweze kuwaheshimu na
kuthamini mchango wao.
Akizungumza
na vijana wakati wa mdahalo wa vijana uliofanyika katika chuo cha
Ufundi (VETA) mkoani Iringa leo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel amesema kuwa
vijana ndio nguvu kazi ya taifa hivyo hawapaswi kulalamika badala yake
washiriki kikamilifu katika kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa
kuyatumia mazingira yanayowazunguka.
Amesema
kuwa tatizo la vijana wengi Tanzania kukabiriwa na changamoto ya
ukosefu wa ajira hasa maeneo ya mijini linatokana na wengi wa vijana
kushindwa kubaini fursa za ajira zilizopo katika mazingira wanayoishi
hivyo kuishia kuilaumu serikali.
Amesema
vijana wengi wanakosa moyo wa kuthubutu kuingia katika biashara halali
za kuweza kuwapatia kipato na kujikuta wakitumia muda mwingi kukaa
viweni na kusubiri serikali iwatafutie ajira jambo ambalo linachangia
vijana wengi kuendelea kuwa maskini.
“Ifike
mahali tukubali kuwa hakuna changamoto yoyote duniani ambayo siyo
fursa,hapa Tanzania yapo maeneo mengi ambayo vijana mkikaa vizuri
mnaweza kutajirika”
Profesa
Elisante amesema kuwa yapo maeneo mengi ambayo vijana wanaweza
kuyatumia wakatajirika huku akiwataka vijana kote nchini walioajiriwa na
kujiajiri kuepuka uvivu na kufanya kazi kwa bidii katika maeneo kazi
yao.
Post a Comment