Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhani Madabida akifungua semina
ya siku 2 iliyoshirikisha Chama Cha Mapinduzi na Chama rafiki cha
Kikomunisti cha China CPC,katika hoteli ya Courtyard mjini Dar es
Salaam, Semina hiyo ilikuwa mahususi katika Kuvijengea Vyama Uwezo na
Umuhimu wa Vijana katika vyama.
Naibu
Mkurugenzi wa CPC katika masuala ya Kimataifa Ndugu An Yuejun akitoa
salaam za shukran kwa niaba ya wajumbe wenzake kabla ya kuanza kwa
semina ya siku mbili iliyoshirikisha CCM na CPC kutoka China.
Profesa
Song Li akitoa elimu juu ya masuala mbali mbali ya kiuchumi ikiwa
mipango iliyofanywa na CPC tangu kuanza kwake katika kuboresha na kukuza
uchumi wa China.
Katibu
Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Ndugu
Anamringi Macha akibadilishana mawazo na Makamu Mkurugenzi katika
masuala ya Kimataifa wa CPC Ndugu An Yuejun mara baada ya kumaliza
semina kwa siku ya kwanza.
Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (Zanzibar) Salama Aboud na Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Bara wakifurahia jambo na Naibu
Mkurugenzi wa masuala ya kimataifa wa CPC Ndugu An Yuenjun.
Katibu
wa Mkoa wa Vyuo Vikuu CCM Ndugu Christopher Ngubiagai akitoa mada juu
umuhimu wa vijana katika CCM na matatizo yanayowakabili vijana wengi wa
Tanzania na kusini mwa jangwa la Sahara katika semina ya siku mbii
iliyoanza tarehe 31 Oktoba na kuhitimishwa tarehe 1 Novemba katika hotel
ya Courtyard jijini Dar es Salaam na kushirikisha vyama viwili marafiki
CCM na CPC kutoka China.
Suleiman
Mwenda kutoka Idara ya Itikadi na Uenezi akielezea namna internet
inavyofanya kazi katika kufikisha ujumbe hasa kwa vijana na pia hatua
ambazo serikali inazichukua katika kuboresha na kuzuia upotoshaji ama
matumizi mabaya ya internet.
Gift
Msuya kutoka Mkoa wa Vyuo Vikuu akifafanua masula mbali mbali yanayohsu
mkoa huo wa vyuo vikuu wakati wa semina ilyoshirikisha CCM na CPC kutoka
China.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ndugu Ramadhani Madabida akitoa mada juu
ya mfumo mzima wa Chama Cha Mapinduzi katika semina ya siku mbili
iliyoshirikisha CCM na CPC kutoka China.
Katibu
Mkuu Msaidizi wa Idara ya Itikadi na Uenezi akiuliza swali linalohusu
ubora wa bidhaa kutoka China wakati wa semina ya siku mbili
iliyohushisha CCM na CPC kutoka China.
Makamu
Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Mboni Mhita akielezea umuhimu wa Umoja wa
Vijana wa CCM katika semina ya siku mbili iliyofanyika katika Hotel ya
Courtyard na kushirikisha vyama viwili marafiki CCM na CPC kutoka China.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhani Madabida akiwa kwenye
picha ya pamoja na viongozi kutoka Chama rafiki cha Kikomunist cha China
pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ndugu Abdilah Mihewa na
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Ndugu Salum Madenge.
Post a Comment