Wafanyakazi wa Idara Mbalimbali wakiwa katika maandamano ya pamoja
kusherehekea sikukuu ya wafanyakazi mwaka huu, Tucta Mkoani mbeya
imepitisha mapendekezo yake ya kima cha chini cha mshahara
****
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) Mkoani Mbeya,
limetangaza kiwango kipya cha mishahara inayotakiwa kuwa kima cha chini
ni Sh 750,000.
Mwenyekiti wa Tucta mkoani hapa, Alinanuswe
Mwakapala alisema kwa maisha ya sasa kima cha chini lazima kiwe
Sh750,000 na kwamba, pendekezo hilo la mkoa litawasilishwa kwenye ngazi
za juu za Tucta ili kulibariki.
Mwakapala alisema hayo kwenye hafla ya Chama cha
Walimu Tanzania (CWT) kukabidhiwa jengo la ghorofa tano lililojengwa na
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
“Wafanyakazi nchini sasa wamechoshwa na mishahara
midogo, hivyo wakati umefika kwa wafanyakazi kutoogopa maandamano na
migomo kudai haki,” alisema huku akishangiliwa.
Hata hivyo, Rais wa CWT, Gratius Mukoba alisema
madai ya wafanyakazi yaliyowasilishwa Serikalini ni kutaka nyongeza ya
mishahara kwa asilimia 100.
Mkoba alisema CWT hivi sasa wanasubiru ndani ya miezi mwili hadi Desemba kupata majibu.
hayatapatikana basi Serikali ijue imejipalia mkaa.
‘’Hatuwezi kuendelea kuwaona watu wasiofanyakazi
wanapata mishahara mikubwa wakati wafanyakazi wanasota. Mwisho wa
matatizo hayo ni sasa’’ alisema huku akiwataka wafanyakazi hususan
walimu kuachana na njama za kutaka kuwatenganisha.
Alisema Serikali inatakiwa kuwalipa walimu Sh49
bilioni wanazodai zikiwamo Sh30 bilioni walizopunjwa katika mishahara na
kwamba pia lazima ipunguze kodi kwa wafanyakazi na kuboresha mazingira
ya kazi
MWANANCHI


Post a Comment