WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi
(pichani) kwa mara nyingine tena wamevaana na Mbunge wa Viti Maalumu, Chiku Abwao
(Chadema), wakati wa mjadala wa mpango wa utekelezaji wa maendeleo
katika Jimbo la Isimani.
Mtafaruku huo ulitokea jana bungeni baada ya Abwao, kuuliza swali la nyongeza kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu, Steven Wassira, ambapo alitaka kujua ni lini vijiji vilivyo katika jimbo hilo vitafikiwa na huduma ya maji safi na salama.
Baada ya kuuliza swali hilo, baadhi ya wabunge walionekana wakivunjika mbavu kwa vicheko huku wengine wakipiga makofi hali iliyomfanya Waziri Lukuvi kutoa majibu ndani ya Bunge huku Abwao akionekana kutokubaliana na majibu hayo.
Kabla ya Lukuvi kunyanyuka na kutoa majibu hayo, Waziri Wassira alisema Serikali imejipanga kuhakikisha vijiji vinapata maji na tatizo hilo si kwa Isimani pekee bali ni maeneo mengi ya nchi.
“Mheshimiwa spika mimi sijasimama kama mbunge wa jimbo, hapa nazungumza kama Serikali kama Waziri na ninayo mamlaka ya kutoa jibu lolote kwa hiyo naomba nieleweke hivyo.
“Serikali inafahamu tatizo la maji katika Jimbo la Ismani na kutokana na kufahamu huko tayari kuna mpango wa mradi wa maji wa Sh bilioni 3 na ukiachia hilo mbunge mwenyewe wa Ismani amekuwa akifanya jitihada mbalimbali za kumaliza tatizo la maji.
“Mpaka sasa visima 25 vya maji vimechimbwa kwa jitihada binafsi za mbunge na mpango mwingine wa kuchimba visima vingine 10 unaendelea,” alisema Lukuvi.
Hata hivyo, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), alisimama kabla ya Spika wa Bunge kuahirisha shughuli za mchana na kuomba mwongozo wa Spika kuhusu hatua ya Lukuvi kutumia kofia mbili kujibu swali ambalo hakuulizwa.
“Nimesimama kwa kanuni ya 68 (7), wakati wa kipindi cha maswali alisimama Lukuvi kujibu swali la Abwao, alijibu akitumia cheo chake cha Ubunge, wakati kanuni ya 39 (1) inatoa ruhusa kwa Waziri kujibu maswali na hoja za wabunge na si wabunge,” alisema Mnyika.
Pamoja na majibu hayo, Spika Makinda, alisema kuwa alichofanya Lukuvi ni sahihi na mbunge yeyote anaweza kukifanya kutumia nguvu ya kujibu.
Alisema jambo hilo linaweza kubadilika ikiwa wabunge wataliingiza katika Katiba kinyume na hivyo hali itabaki kuwa kama ilivyo.

Post a Comment