Mzee Kitwana Kondo akiongea na Mjumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, Emmanuel John walipokutana msibani Kibada hivi karibuni |
******
MWANASIASA mkongwe na Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam,
Kitwana Kondo (88), amelazwa katika Hospitali ya Hindu Mandal, kutokana
na kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi. Kitwana Kondo maarufu wa jina la
‘KK’ alipatwa na maradhi hayo mwezi mmoja uliopita, hali iliyosababisha
kukimbizwa hospitalini huku akiwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji
uangalizi maalumu (ICU), kwa ajili ya matibabu zaidi.
Akizungumza na RAI jana mtoto mkubwa wa kiume wa mwanasiasa huyo, Adinan Kondo, alisema kuwa mzee wao alipatwa na maradhi hayo hali iliyowalazimu kumkimbiza hospitali.
Alisema katika kipindi cha muda wa wiki tatu mzee Kitwana Kondo, alipoteza fahamu na alikuwa hamjui anayeingia wala anayetoka lakini hali ilibadilika kuanzia juzi kwa kuanza kuvuta hisia na kujigeuza huku akiwa kitandani.
Akizungumza na RAI jana mtoto mkubwa wa kiume wa mwanasiasa huyo, Adinan Kondo, alisema kuwa mzee wao alipatwa na maradhi hayo hali iliyowalazimu kumkimbiza hospitali.
Alisema katika kipindi cha muda wa wiki tatu mzee Kitwana Kondo, alipoteza fahamu na alikuwa hamjui anayeingia wala anayetoka lakini hali ilibadilika kuanzia juzi kwa kuanza kuvuta hisia na kujigeuza huku akiwa kitandani.
“Hali ya mzee imekuwa ikibadilika tofauti na siku za mwanzo tulizomleta hapa hospitali, kwani hali ilikuwa mbaya zaidi alikuwa hamjui anayeingia wala anayetoka lakini kwa muda wa siku mbili hizi ameanza kupata nafuu na kuweza kujigeuza kwa mbali ingawa bado yuko kitandani.
“Pamoja na hali yake hiyo, lakini bado anakula kwa kutumia mipira maalumu kwani hawezi kukaa mwenyewe na kubwa tunamuomba Mwenyezi Mungu azidi kumpa nafuu mzee wetu ili arejee katika hali yake ya kawaida,” alisema Adinan.
Adinan aliwashukuru viongozi wa Serikali ambao kila mara wamekuwa wakifika hospitalini hapo kumjulia hali mwanasiasa huyo mstaafu ambaye alikubalika na makundi mbalimbali.
Alisema miongoni mwa viongozi ambao wamefika kumuona hadi sasa ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, ambaye muda wote amekuwa akishinda hospitalini hapo.
“Viongozi mbalimbali wamekuwa wakija kumjulia hali akiwemo mzee Mwinyi, ambaye ni rafiki mkubwa wa mzee kila siku tupo naye hapa hospital, mbali na yeye pia mzee Kingunge Ngombale Mwiru anakuja,” alisema.
Adinan pia alisema, Rais Jakaya Kikwete aliporudi kutoka Marekani alienda moja kwa moja hospitalini hapo kumuona mgonjwa na hata kuifariji familia.
“Ninachotaka kusema ninawaomba Watanzania wazidi kumuombea mzee Kitwana Kondo ili arudi katika hali yake ya kawaida. Ni mengi ameyafanya katika nchi hii nadhani kila mtu anafahamu, Kitwana Kondo ni nani ndani ya ardhi ya Tanzania,” alisema mtoto huyo.
Hata hivyo, Adnan alishangazwa na kitendo cha mameya wa Dar es Salaam, ambao licha ya kupewa taarifa za ugonjwa wa mzee huyo lakini wameshindwa kwenda kumjulia hali.
Alisema baadhi yao kabla ya kuomba nafasi hizo walikuwa wakienda nyumbani kwa Kitwana Kondo kwa ajili ya kuomba ushauri wake, lakini wameshindwa kumjali baada ya kuugua.
“Ninachotaka kusema kwa mameya hawa pamoja na manispaa zote tatu, wajue kwamba hata kama watakuja kwa sasa hawatopata nafasi ya kumuona mzee. Kwani tangu siku ya kwanza nimewapigia kila mmoja na kumwambia lakini inaonekana mzee wetu kwao hana thamani,” alisema Adnan.
Kitwana Kondo, ni moja ya wanasiasa mashuhuri nchini ambaye aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na baadaye kuukwaa ubunge wa Kigamboni kuanzia mwaka 1995 hadi 2000 kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, alishindwa kutetea nafasi yake kwa kubwagwa na Frank Magoba wa Chama cha Wananchi (CUF), ambaye kwa sasa amejiunga na CCM.
Februari 2, 1999 Kitwana Kondo akiwa Mbunge wa Kigamboni, alisimama ndani ya Bunge na kutoa hoja ya kuitaka Serikali iondoe kero zinazowasibu Waislamu na makundi yote ya wanaharakati ya Kiislamu.
Itakumbukwa miaka ya 1990 alikuwa ni mmoja wa kiongozi aliyezima uvunjwaji wa mabucha ya nguruwe katika eneo la Kigogo kwa kuweza kufanya mazungumzo na viongozi wa dini ya Kiislamu akiwemo marehemu Sheikh Kassim Bin Jumaa, aliyekuwa imamu wa Msikiti wa Mtoro.
RAI
Post a Comment