Dk. Azavery Lwaitama |
BAADHI ya wadau wa elimu nchini, wameponda utaratibu wa Serikali
kupunguza alama za ufaulu kwa mtihani wa kidato cha nne na sita na
kusema hatua hiyo imefanywa kwa lengo la kuwafurahisha wanasiasa. Baadhi
ya wanazuoni waliozungumza na RAI, walisema kuwa hatua hiyo haiwezi
kuondoa tatizo la wanafunzi wa shule za umma wanaoshindwa kufaulu
vizuri.
Mhadhiri Mwandamizi mstaafu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk. Azavery Lwaitama alisema jana kuwa daraja la sifuri, kulibadilisha jina na kuliita daraja la tano imefanywa kwa lengo la kuinusuru Serikali isizomewe.
Dk. Lwaitama alisema waliotengeneza madaraja hayo wamefanya hivyo kwa ajili ya kutekeleza matakwa ya wanasiasa kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
Alisema Serikali inapaswa kutambua kuwa alama si hoja na kusisitiza jambo la msingi kuwekeza katika elimu, wakaguzi wa shule kufanya ukaguzi endelevu, kuwapiga msasa walimu pamoja na kuwapo mikutano ya mara kwa mara ya walimu wa masomo.
‘Ninyi mnataka Serikali izomewe, ndiyo msingi wa kuliita daraja la sifuri kuwa daraja la tano… hii ni lugha nzuri tu, lakini tuwekeze kwenye elimu, alama si elimu.
“Tuwekeze katika walimu, siyo kwa wabunge hapo italeta lugha nzuri, mwisho tutasema waliopata daraja la tano ni wengi kuliko daraja la kwanza,” alisema, Dk. Lwaitama.
Naye, Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Alli, alisema matatizo ya msingi ya elimu hayawezi kutatuliwa kwa kuwatahini wanafunzi.
Alli alisema mabadiliko yaliyofanywa kupunguza alama za ufaulu hayawezi kuleta mabadiliko yoyote iwapo hayatokuwapo mabadiliko katika kujifunza na kufundisha.
Alisema mfumo wa ufundishaji hasa katika shule za umma ni mbovu ambao unawafanya wanafunzi kutosoma na kuhoji wanafunzi hao wataweza kutahiniwa vipi?
Alli alisifia mfumo wa ufundishaji katika shule za watu binafsi, kwa kusema waliwahi katika mfumo wa elimu kwa kutoa mitihani yao inayowachuja wanafunzi wenye uwezo na wasio na uwezo.
“Tunahitaji mwongozo mzuri katika kufundisha, nguvu zaidi zielekezwe katika shule za umma ambazo ni dhaifu…. wengine watasema kwanini sasa, ndio tunaelekea kwenye uchaguzi wa 2015.
“Pengine haya ndio maamuzi ya wataalamu wetu, mfumo wa taaluma umefanya kazi yake, lakini mimi nasema mfumo wa kufundisha ni mbovu na ufanye kazi yake.
“Wanafunzi wa shule za umma wanahitaji mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishwa,” alisema Alli.
Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Kitila Mkumbo alisema kitendo hicho ni kama kuzunguka mbuyu na kuna kitu inaficha juu ya matokeo hayo.
Dk. Kitila alisema kuwa kubadilisha madaraja ya matokeo si suluhisho bali suluhisho ni kuboresha mazingira ya kufundishia wanafunzi.
“Hapa tatizo ni jinsi wanafunzi wanavyofundishwa, nimesikitika kuona Serikali inafuta daraja la nne ambalo ni ziro na kuliita kwamba ni ufaulu dhaifu, hii ni lugha ya kihuni.
“Hatuwezi kuboresha elimu kwa kucheza na mabadiliko ya madaraja, hatuwezi kuwa na matokeo makubwa bila kufanya kazi kubwa ya kuboresha mazingira na ufundishaji.
“Huu ni mchezo wa kuigiza, naomba Serikali itambue kwamba tatizo lililopo ni udhaifu wa ufundishaji na wafundishaji na si madaraja ya ufaulu, kwanza mfumo wa Grade Point Average (GPA) tulikuwa nao ukatushinda,” alisema.
Naye, Mchumi Mwandamizi wa Chuo cha Mzumbe, Dk. Honest Ngowi alisema kuwa kilichofanywa na Serikali ni kuandaa wingi wa wanafunzi waliofaulu, lakini hawana ubora.
Akizungumza na RAI akiwa nchini Australia, Dk. Ngowi alisema kilichofanywa na Serikali ni kuendelea kudhoofisha kizazi cha sasa kwa kuwa hakitaweza kuhimili ushindani katika Afrika na dunia katika elimu na uchumi.
“Ingekuwa bora kuboresha mazingira ya kusomea na kufundishia ili wafaulu katika viwango vya zamani, haifai kushusha kimo cha goli ili golikipa mfupi aweze kufikia, ni vema likabaki vile vile ili aweze kuruka,” alisema.
Naye, Mwalimu wa taaluma Shule ya Sekondari ya Rosmini jijini Tanga, Ahmed Mmombo, alisema utaratibu huo umelenga kuzibeba shule za kata zilizojengwa kisiasa na ambazo hazifanyi vizuri.
Mmombo alisema Serikali imeona kuendelea na utaratibu wa zamani ungewaharibia zaidi katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
“Wamejijengea kwa ajili ya uchaguzi wa 2015, lakini reality (ukweli) haiko hivyo, elimu yetu itadharauliwa watoto wetu wakitoka nje wataonekana ni dhaifu sana.
Hatua ya Serikali kupunguza alama za ufaulu mtihani wa kidato cha nne na sita, imekuja ikiwa imebaki siku moja tu kwa wanafunzi wa kidato cha nne nchini kote kuanza mtihani wa kumaliza ngazi hiyo ya elimu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome, alisema juzi kuwa, mtihani wa taifa wa kidato cha nne na sita utakuwa na alama 60 za ufaulu alama 40 zilizobaki zitatokana na zile za maendeleo ya mwanafunzi shuleni (CA). Mfumo huu mpya utaanza kutumika katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka huu.
RAI

Post a Comment