![]() |
| Marehemu Francis Shumira |
MAJERUHI Francis Shumira aliyejeruhiwa katika tukio la kushambuliwa kwa
risasi Ilala Dar es salaam jana amefariki dunia leo asubuhi Hospitali ya
Muhimbili alikolazwa MOI kwa matibabu.
Kufariki kwa Francis kunafanya idadi ya watu waliofariki katika tukio
hilo hadi hivi sasa huku ikiacha majeruhi wawili mmoja Christina Alfred
Newa Mwanafunzi wa masuala ya Mawasiliano visiwa vya Syprus na mama
mzazi wa Christina, Hellen Elieza Newa.
Aidha mipango ya mazishi ya mtumishi wa Benki ya Barclays ya jijini Dar
es Salaam, Alfa Alfred Newa inafanyika nyumbani kwao Ilala karibu na
Kablu ya wazee huku maziko yakisubiri kutengemaa kwa afya ya mama mzazi.
Familia imekiri kuwa Christina na Marehemu Munisi walikuwa na mahusiano
lakini ni zamani na walitengana kutokana na vurugu alizowahi mfanyia
siku za nyuma.
IKUMBUKWE Tukio la shambulizi la risasi lililotokea hii Novemba 19, 2013
asubuhi Ilala Amana jirani na Hoteli ya MM na Klabu maarufu ya wazee
limesababisha vifo vya watu wawili na kuacha majeruhi watatu wawili kati
yao wakiwa taabani.
Taarifa za awali za Polisi zinapasha kuwa, Watu walio poteza maisha
katika tukio hilo ambalo lilikuwa ni la mtu aliyetambulika kwa jila la
Godfrey Munisi kuwapiga risasi wana familia lilisababisha kifo cha Alfa
Alfred na liliwajeruhi Francis Khiranga Shumira , Christina Alfred,
Hellen Elieza Newa.
Taarifa hizo zinasema kuwa Mfyatua risasi huyo ambaye baade alijiua
nayeye, Godfrey Munisi alikuwa na uhusiano wa karibu na Christina Alfred
Newa.
Katika tukio hilo, ambalo linaelezwa kuto tofautiana sana na lile la
Mwanahabari ufoo Saro lililotokea miezi ya hivi karibuni, muuaji
alimjeruhi Nshumila kifuani na mama yake Christina alijeruhiwa maeneo
ya begani na hali zao siyo nzuri na wamelazwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
Huku Christina akijeruhiwa mkononi na mguuni ambapo alitibiwa katika
Hospitali ya Amana na Kuruhusiwa kurudi nyumbani huku mdogo wa
Christina, Alfa Alfred akifariki kabla ya kufikishwa Hospitali.
Marehemu Alfa Alfred Newa pia alikuwa wa benki ya Barclays ya jijini
Dar es Salaam. Shumira ni baharia kitaaluma na inaelezwa kuwa ni raia wa
Kenya.
Source: Father Kidevu Blog



Post a Comment