Vijana
milioni 2.6 wenye umri wa miaka kati 15 na 24 nchini, wanaishi na
virusi vya Ukimwi. Takwimu hizo zilitolewa jana jijini Dar es Salaam na
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(Unesco), Abdoul Coulibaly, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya elimu ya
jinsia na afya ya uzazi kwa vijana katika nchi 21 za Mashariki na Kusini
mwa Afrika.
Alisema karibu vijana 50 katika nchi hizo huambukizwa virusi vya Ukimwi
kila saa moja, huku idadi ya wasichana wakiongoza kwa maambukizi hayo. Coulibaly
alisema idadi hiyo ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa vijana kwa
Tanzania, inachangiwa na kutokuwapo kwa elimu ya kutosha ya jinsia
pamoja na VVU na Ukimwi, afya ya uzazi na ukuaji wa binadamu.
Alisema asilimia kubwa ya vijana hawana uelewa wa masuala ya afya ya
uzazi na jinsia, jambo ambalo husababisha kujiingiza kwenye mapenzi
katika umri mdogo na kusababisha kuongezeka kwa mimba za utotoni.
Pia aliiomba serikali kuweka mikakati madhubuti ya kutoa elimu ya afya
na jinsia kwa vijana kwa ajili ya kusaidia kupunguza idadi ya maambukizi
kwao pamoja na mimba za utotoni zinazosababishwa na ukosefu wa elimu
hiyo.
Kaimu Mkurugenzi, kitengo cha masuala mtambuka kutoka Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Laetitia Sayi, alisema changamoto ya maambukizi ya
VVU kwa vijana ni kubwa na kwamba serikali kwa upande wake inafanya
jitihada mbalimbali za kutatua tatizo hilo.
credit: JF
Loading...
Home » Unlabelled » Mamilioni ya vijana nchini wanaishi na VVU - Wasichana wanaongoza kwa maambukizi
Post a Comment