|
Eneo la TRA, jijini Arusha. |
Toka jana jioni wakazi wa jiji la Arusha wameendelea kuwa katika
taharuki na minong'ono hapa na pale kutokana na tukio la kupigwa risasi
binti mmoja aitwaye Violeth Mathias katika ofisi za TRA Arusha.
Mwanadada huyu aliyeonesha jeuri ambayo haikutegemea si tu Arusha bali
katika Taifa hili hasa lile la kwenda na kuchukua Bastola na kutaka
kummaliza askari aliyekuwa akitimiza wajibu wake katika Bank ya CRDB.
Kitendo hiki kimelfanya wakazi wa jiji hili kuwa na Maswali mengi kuliko
majibu. Hasa juu ya anakota jeuri ama kiburi mwanadada huyu.
Viola alikwenda CRDB kuchukua pesa na kilichotokea yeye alipaki gari
eneo lisiloruhusiwa kwa mazingira yale ya Bank. Hivyo askari Polisi
alimfuata na kumwelekeza kwamba haruhusiwi kupaki gari eneo hilo ila
yeye (Mwanadada) huyu hakutaka kusikiliza alichokuwa akiambiwa. Akashuka
na kwenda bank ndani.
Hata hivyo Polisi alimfuata ndani ila cha kushanga mwanamke huyu akagoma
tena. Ndipo Polisi kwa ajili ya usalama alirudi nje na kutoa upepo
matairi yote ya gari kwa tahadhari. Cha kustaajabisha ni pale binti huyo
aliporudi na kukuta hali hiyo alipoulizwa alijibiwa polisi ndiye
aliyefanya hivyo. Alichofanya alienda kwenye gari lake na kutoka na
bastola ati akitaka kumlenga yule askari polisi ndipo yule askari
alipoaamu kujihami na kumshut begani.
Baada ya watu kuchunguza wakajua kuwa kiburi hicho anakitia kwa RC wa
Arusha Bwa. Magesa Mulongo kwa kuwa anajipumzisha kwake. Wakazi wengi wa
hapa wameshangazwa sana namna RC anavyozidi kuchafua nafasi yake hiyo
na hata yule aliyempatia.
Cha kusikitisha zaidi ni RPC kuamua kukimbia waandishi wa habari baada
ya waandishi kumfuata na kumtaka atoe maelezo juu ya hilo tukio. RPC
kuona waandishi wa habari alimwamuru dereva kugeuza gari na kuondoka
jambo lililopelekea waandishi wa habari kuamini kuwa RPC atakuwa
amepokea maeleekezo toka kwa RC.
RPC alipopigiwa simu aliishia kusema anaelekea Hospitali kwa kuwa Sukari
yake haiko sawa hili limepelekea kuaminika kuwa Mulongo anawaweka
viongozi wenzie katika wakati mgumu kutokana na tabia zake hizi.
Credit: JF
on Thursday, October 31, 2013
Post a Comment