Afisa
Afya Usafishaji toka Manispaa ya Temeke Ernest Mamuya akieleza kwa
waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusu hatua mbalimbali
zinazochukuliwa na manispaa katika kukabiliana na wachafuzi wa mazingira
ikiwa ni pamoja na kutozwa faini isiyopungua 50,000,wakati wa mkutano
uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).katikati ni Afisa
Afya Mazingira wa Manispaa hiyo Bw. Willium Muhemu na mwisho ni Afisa
Habari wa Manispaa hiyo Bi.Lynn Chawala.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiwasikiliza wawasilishaji toka Manispaa ya Temeke.
Afisa
Afya Mazingira toka Manispaa ya Temeke Bw. Willium Muhemu akieleza kwa
waandishi wa Habari (hawapo pichani) mikakati mbalimbali ya Manispaa
hiyo inayotumika katika kuhakikisha wakazi wa manispaa husika
wanatekeleza sheria na kanuni za afya zilizoweka ,wakati wa mkutano
uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).Kulia ni Afisa
Habari wa Manispaa hiyo Bi.Lynn Chawala.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
Na Frank Mvungi Maelezo
Halmashauri
ya Manispaa ya Temeke yatenga zaidi ya shilingi milioni 434 katika
bajeti ya 2013/2014 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya usafi wa
mazingira.
Hayo
yamesemwa naAfisa Afya Mkuu wa Manispaa ya Temeke Bw. Ernest Mamuya
leo Jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari
uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO.
Alisema
manispaa hiyo imeweza kuendesha ukaguzi katika maeneo ya kutolea
huduma kama hoteli na katika makazi ya watu ili kuwabaini wanaochafua
mazingira.
Katika
kufanikaisha suala la usafi katika manispaa hiyo vifaa
vitakavyonunuliwa ni Compactor 1,tela moja la futi 40 kwa ajili ya
usafirishaji taka,ununuzi wa mashine 3 za kusafishia barabara,kununua
gari 1 la maji taka na kujenga vizimba 3 vya kuhifadhia taka kwa muda.
Ambapo
katika kuhakikisha halmashauri inaongeza kiwango cha udhibiti taka na
kuboresha hali ya usafi halmashauri imenunua malori mapya 3 aina ya TATA
katika bajeti ya 2012/2013 ambayo yaligharimu milioni 324.
Bw.
Mamuya alibainisha kuwa manispaa hiyo ina mikakati mbalimbali ikiwemo
kusafisha maeneo muhimu ikiwa ni pamoja na barabara kuu,maeneo ya wazi,
masoko, mifereji na kuongeza uwezo wa kukusanya taka,kuzihifadhi na
kuzisafirisha kwenda dampo.
Alisema
kuwa Mkakati mwingine ni kuelimisha na kuhamasisha jamii ili iweze
kuunga mkono na kushiriki katika kuweka mazingira katika hali ya usafi.
Aliongeza
kuwa Halmashauri hiyo imefanikiwa kuzuia magonjwa ya milipuko kwa
kipindi cha miaka mitatu mfululizo kufuatia mikakati kabambe ya
kuhamasisha na kusimamia usafi wa Mazingira katika ngazi ya Kaya na
kuigawa halmashauri hiyo katika kanda 5 za ufuatiliji na usimamizi wa
usafi wa mazingira ili kurahisisha kazi ya ufuatiliaji na usimamizi wa
usafi.
Naye
Afisa Habari wa Manispaa ya Temeke Lynn Chawala alisema Manispaa hiyo
inatarajia kubadili utaratibu wa kutupa taka dampo la pugu na kwenda
kutupa Kisarawe II ambapo ni karibu zaidi hali itakayopunguza gharama
za kusafirisha taka.
Post a Comment