Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSPF ambaye pia ni
Meneja wa kumbukumbu, Chacha Nyaikwabe
Meneja wa kumbukumbu, Chacha Nyaikwabe
Kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano, Masoko na
Uenezi wa PSPF, Hawa Kikeke, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSPF ambaye pia ni
Meneja wa kumbukumbu, Chacha Nyaikwabe na Frank Mvungi wa Maelezo wakati PSPF
ilipozungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa habari maelezo
Uenezi wa PSPF, Hawa Kikeke, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSPF ambaye pia ni
Meneja wa kumbukumbu, Chacha Nyaikwabe na Frank Mvungi wa Maelezo wakati PSPF
ilipozungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa habari maelezo
Waandishi wa habari wakisikiliza ufafanuzi kuhusu
mfuko wa pensheni PSPF.
mfuko wa pensheni PSPF.
Kutoka
kushoto ni Afisa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Hawa Kikeke,
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSPF ambaye pia ni Meneja wa kumbukumbu,
Chacha Nyaikwabe
*********************
Waandishi
wa habari nchini wameshauriwa kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari
(PSPF Supplementary Scheme PSS) katika Mfuko wa pesheni wa PSPF ili
kujiwekea akiba yenye mafao bora na itakayowainua kiuchumi.
Wito
huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSPF ambaye pia ni
Meneja wa kumbukumbu, Chacha Nyaikwabe wakati akizungumza na waandishi
wa habari kwenye ukumbi wa habari maelezo Novemba 19 mwaka huu.
Nyaikwabe
amesema mpango wa uchangiaji wa hiari ni msaada mkubwa kwa watu wote
walio na wasio katika sekta rasmi ambao kwa kujiunga na mpango huo
watanufaika na mafao ya elimu, ugonjwa, ujasiliamali, fao la uzeeni,
kujitoa na mkopo wa nyumba kwa wale watakaokidhi vigezo.
“PSPF
sasa ni kwa watu wote walio kwenye sekta rasmi na wale ambao hawako
kwenye sekta rasmi maana lengo letu ni kuwafikia watu wengi ndani na nje
ya nchi kupitia mpango huu wa uchangiaji wa hiari PSS ambao kiwango
chake cha chini cha uchangiaji ni sh.10,000 kwa mwezi” anasema
Nyaikwabe.
Akizungumzia
mwamko wa watu kujiunga na mpango huo wa hiari PSS, Nyaikwabe amesema
kumekuwa na mafanikio makubwa kwani tangu kuzinduliwa kwake mapema machi
7 mwaka huu tayari wanachama zaidi ya 2000 wamejiunga na mpango huo.
Kwa
upande wake Afisa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Hawa Kikeke
watu wengi wanajiunga na mfuko huo kutokana na ubora wa mafao yake na
mikopo inayotolewa kwa wanachama waliojiunga na mfuko huo kwa miaka
mitano tofauti na wakati wa nyuma ambapo mikopo ya nyumba ilitolewa kwa
wanachama waliobakiza miaka mitano ya kustaafu.


Post a Comment