Ufoo Saro akiwa hospitali baada ya kupigwa risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther Mushi. |
SIKU chache baada ya Mtangazaji wa Runinga ya ITV, Ufoo Saro
kuruhusiwa hospitalini alipokuwa amelazwa baada ya kudaiwa kupigwa
risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther Mushi, ameibuka na kula kiapo
cha siri.
Ufoo ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,
katika tukio la yeye kupigwa risasi, alimpoteza mama yake mzazi aitwaye
Anastazia Saro…
Stori:Brighton Masalu na Chande Abdallah
SIKU chache baada ya Mtangazaji wa Runinga ya ITV, Ufoo Saro kuruhusiwa hospitalini alipokuwa amelazwa baada ya kudaiwa kupigwa risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther Mushi, ameibuka na kula kiapo cha siri.
SIKU chache baada ya Mtangazaji wa Runinga ya ITV, Ufoo Saro kuruhusiwa hospitalini alipokuwa amelazwa baada ya kudaiwa kupigwa risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther Mushi, ameibuka na kula kiapo cha siri.
Ufoo ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,
katika tukio la yeye kupigwa risasi, alimpoteza mama yake mzazi aitwaye
Anastazia Saro aliyedaiwa kuuawa na marehemu Mushi aliyejiua kwa risasi.
Akizungumza na gazeti hili Ufoo alisema, kamwe hawezi kusema
kilichokuwa kikiwagombanisha yeye na marehemu Mushi mpaka siku ya mwisho
wa uhai wake.
Ufoo Saro.
“Siwezi kuzungumzia kabisa chanzo wala ugomvi wetu mimi na marehemu Mushi. Hiyo itakuwa siri yangu,” alisema Ufoo.
Katika mahojiano na gazeti hili, mtangazaji huyo alipoulizwa kuhusu
msimamo wake wa uhusiano baada ya kupona kabisa alisema, hawezi
kujiingiza tena kwenye mapenzi kwa sasa.
“Sitaki kabisa kusikia juu ya mapenzi, siwezi kuliweka suala hilo
akilini tena,” alijibu kwa kifupi kwa sauti ya chini lakini yenye mkazo.
GPL
Post a Comment