Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
MABINGWA
watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ya jijini Dar
es salaama wamebarizi kieleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara
kufuatia ushindi wa mabao 4-0 kwenye uwanja wa Taifa jioni hii dhidi ya
timu iliyoanza ligi kwa kishindo, lakini kwa sasa mambo ni mdobwedo
kwao, JKT Ruvu ya mkoani Pwani.
Ushindi
huo muhimu inaifanya Yanga kufikikisha pointi 25, tofauti na timu mbili
za Azam fc na Mbeya City zenye pointi 23 kila moja, lakini yawezekana
Yanga wakaa kileleni kwa saa tu endapo timu hizo zitashinda katika
michezo yao ya wikiendi hii.
Mabao
ya Yanga leo hii yamefungwa na winga hatari wa klabu hiyo, Mrisho
Khalfan Ngassa aliyefunga mawili ambapo katika dakika ya tatu alipiga
shuti kali baada ya kufanikiwa kuwachomoka walinzi wa JKT Ruvu na
dakika ya 12 aliunganisha kama kawaida mpira wa kurusha wa beki Mbuyu
Twite na kuleta shangwe kubwa kwa mashabiki waliofurika uwanjani.
Mpaka
dakika 45 za kipindi cha kwanza zikimalizika, Yanga walikuwa nyuma kwa
mabao 2-0, lakini kiukweli JKT Ruvu ndio walicheza soka zuri na la
uhakika, ila Yanga waliwazidi kwa hesabu nzuri za mashambulizi ya
haraka.
Kipindi
cha pili kilipoanza, Yanga waliendelea kulisakama lango la JKT Ruvu na
Beki Oscar Samwel Joshua aliandika bao la tatu dakika ya pili ya
kipindi cha pili akiunganisha kona murua iliyochongwa na winga mwenye
kasi kubwa, Simon Msuva.
Karamu ya mabao kwa Yanga leo hii ilikamilishwa na Jerryson John
Tegete baada ya kuzamisha gozi kambani katika dakika ya 89 na
kuwafanya mashabiki wa klabu hiyo waamshe mzimu wa kebehi kwa mashabiki
wa timu Pinzania ya Simba ambayo jana ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Wana
`Nkulukumbi` Kagera Sugar na mashabiki kufanya fuja na kunyofoa baadhi
ya viti vya uwanja wa Taifa.
Kikosi
cha Yanga SC: Deo Munishi ‘Dida’, Mbuyu Twite/Ibrahim Job dk45, Oscar
Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan/Relianst Lusajo dk78,
Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier
Kavumbangu/Jerry Tegete dk64, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza.
Kikosi cha JKT Ruvu; Sadick Mecks, Mussa Zuberi, Kessy Mapande, Omar Mtaki, Damas Makwaya/Richard Msenyi dk64, Nashon Naftali, Amos Mgisa, Haruna Adolph, Paul Ndauka, Samuel Kamutu/Abdallah Bunu dk 64 na Sosthenes Manyasi/Emmanuel Pius dk59.
Kikosi cha JKT Ruvu; Sadick Mecks, Mussa Zuberi, Kessy Mapande, Omar Mtaki, Damas Makwaya/Richard Msenyi dk64, Nashon Naftali, Amos Mgisa, Haruna Adolph, Paul Ndauka, Samuel Kamutu/Abdallah Bunu dk 64 na Sosthenes Manyasi/Emmanuel Pius dk59.
Raundi
ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambayo ipo katika raundi yake ya 12
inaendelea kesho (Novemba 2 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazochezwa
katika miji minne tofauti.
Mgambo
Shooting na Coastal Union zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga, Mbeya City na Ashanti United zitaumana kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex,
Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu,
Morogoro).
Raundi
hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Tanzania
Prisons itakuwa mwenyeji wa Oljoro kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya.
Mechi
za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7
mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashanti United vs
Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, na Ruvu Shooting vs Mtibwa
Sugar.
Novemba
7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro JKT
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa
Tanzania Prisons.
Post a Comment