Wafugaji wa kijiji cha Kambala Wilaya ya Mvomero wakiwa katika mmkutano na Kituo cha haki za binadamu..
mgogoro
wa ardhi uliopo baina ya wakulima na wafugaji wa vijiji vya Dihombo,
Mkindo na Kambala Wilayani Mvomero kituo cha kisheria na haki za
binadamu (LHRC) kimeingilia kati kwa kusikiliza madai ya pande hizo
mbili lengo likiwa ni kutafuta chanzo cha mgogoro huo ili wahusika
waweze kuutafutia ufumbuzi wa kudumu.Timu ya wataalamu wa sheria
na haki za binadamu jana walifika katika kijiji cha Kambala ambacho
kinadaiwa kuwa ni kijiji cha wafugaji na baadaye kufika katika kijiji
cha Dihombo na Mkindo ambavyo navyo vinadaiwa kuwa ni vijiji vya
wakulima na kufanya mazungumza na uongozi wa jamii hizo wa wafugaji na
wakulima.
Katika
mazungumzo hayo pande hizo mbili zilidai wa mgogoro huo umetokana na
kugombea bonde la mto Mgongola ambalo limekuwa likitumiwa na wakulima
pamoja na wafugaji kwa kipindi kwa miaka mingi iliyopita ambapo kwa sasa
limekuwa likigombewa na kila upande ukidai kuwa na haki ya kumiliki.
Akizungumza
mbele ya wataalamu hao kutoka LHRC Emanuel Ibrahimu ambaye ni mfugaji
wa jamii hiyo ya kimasai alisema kuwa anashangazwa na kauli za wakulima
pamoja na baadhi ya viongozi wa Wilaya na hata mkoa wanaodai kuwa bonde
hilo na mgongola ni mali yao wakati wafugaji ndio wenye haki ya kumiliki
bonde hilo kisheria.
Mchngaji wa Kanisa la KKKT wilaya ya mvomero ambaye nae ni mfugaji akielezajambo kuhusu Mgogoro huo.
Kiongozi wa Wafugaji akielezea kuhusu mgogoro wa wakulima na wafugaji katika Bonde la Mgongola Wialaya ya Mvomero.Alisema
kuwa miaka iliyopita walikuwa wakifanya shughuli ya ufugaji huku
wakulima nao wakifanya shughuli ya kilimo bila ya kuwepo kwa migogoro
lakini baada ya kuibuka kwa wakulima wakubwa kutoka maeneo ya nje ya
Wilaya hiyo wengine wakitokea mikoa ya jirani ndipo mgogoro huo
ulipoanza na kwamba kwa sasa umefikia katika hatua mbaya kwani baadhi ya
viongozi wamekuwa wakiwakingia kifua wakulima hao.
Kufuatia
hali hiyo wafugaji hao walisema kuwa wako tayari kumwaga damu na hata
kuuana mpaka wahakikishe kuwa bonde hilo limerudi katika mikono ya
wafugaji ambao ndio wenye uhalali walimiki kisheria na kwamba bonde hilo
wanalitegemea kwa kulishia mifugo na na kupata maji.
Hata
hivyo aliutaja mtanadao wa vikundi vya wakulima nchini MVIWATA kuwa nao
ni moja ya chanzo cha mgogoro huo na pia baadhi ya viongozi wa wilaya
wamekuwa wakitoa maneno ya kejeri kwa wafugaji hali ambayo walidai kuwa
inaonesha wazi kuchukiwa na serikali.
Kwa
upande wao baadhi ya wakulima wa vijiji vya Dihombo na Mkindo walisea
kuwa wao ndio waanzilishi wa bonde hilo na ndio waliowakaribisha
wafugaji katika maeneo hayo na kwamba wafugaji ni wavamizi katika bonde
hilo.
Pascal
Boniface ambaye ni mkulima aliiomba serikali kutafuta suluhisho la
mgogoro huo unaoweza kugharimu maisha ya watu wengi kwani wafuagi na
wakulima tayari wamejiandaa kwa mapigano hali ambayo inatishia usalama
na kwamba shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo hayo zimesimama
huku watoto wakishindwa kwenda shule wakihofia kuuawa.
Akitoa
majumuisho na ufafanuzi mara baada ya ziara hiyo ya HLRC Afisa wa
dawati la kufuatia ukiukwaji wa haki za binadamu Mkuta Masole alisema
kuwa ni vyema Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine ikaukatafutia
ufumbuzi wa haraka mgogoro huo kwani kutokana na mgogoro huo zipo baadhi
ya haki za minadamu zinavunjwa ikiwepo haki ya mtoto kwenda shule.
Aidha
aliliomba jeshi la polisi kuhakikisha maeneo hayo yanalindwa wakati
wote katika kipindi hiki cha mgogoro ili kudhibiti matukio ya mauaji na
uvunjifu mwingine wa amani ambao unaweza kutokea huku akisema kuwa yote
waliyoelezwa na pande hizo mbili yatafanyiwa kazi na kutolewa taarifa
kwa umma ili kuisaidia serikali kutatua mgogoro huo.
Post a Comment