Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LOWASSA KUKUTANA NA BODABODA LEO

 


 
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, anatarajia kukutana na Kamati Kuu ya shirikisho la bodaboda Saccos kwa ajili ya ufunguzi wa Saccos hiyo.

Ufunguzi huo unatarajia kufanyika Leo jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni pamoja na kuwakwamua kiuchumi madereva bodaboda nchini.

Ofisa habari wa Chama cha bodaboda mkoa wa Ilala, Abdallah Bakari, alimshukuru Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM), kwa kutambua umuhimu na uwepo wa bodaboda na kwamba ni mfano wa kuigwa na viongozi wengine.

Bakari amewataka viongozi wengine kuiga mfano huo na kuwasaidia vijana ili kuwawezesha kuinua vipato vyao na kuwawezesha pia kimiliki pikipiki na kuondoa matatizo yanayojitokeza.




Pia, ameziomba asasi na watu mbalimbali kuwasaidia madereva bodaboda walioko hospitalini kutokana na ajali, kupata matibabu ili waweze kurejea kazini kwani wamekuwa wakikaa kwa kipindi kirefu bila kupatiwa matibabu na wengine kufariki.

Madereva hao pia wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za barabara ili kupunguza ajali. 


CHANZO: NIPASHE
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top