Hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo itatoa hukumu
dhidi ya kesi ya kukutwa na simu gerezani inayomkabili Mkurugenzi wa
zamani wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
Amatus Liyumba. Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi,
Augustina Mmbando baada ya kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka na
utetezi wa Liyumba na kupitia majumuisho ya mwisho yaliyowasilishwa na
pande zote mbili kuomba mshtakiwa aonekane ana hatia ama la.
Katika kesi hiyo, Liyumba anadaiwa kukutwa na simu
akiwa Gereza la Ukonga Dar es Salaam, wakati akitumikia kifungo cha
miaka miwili kilichotokana na kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya
ofisi ya umma. Inadaiwa kuwa, Julai 27 mwaka 2011 katika Gereza la
Ukonga, Liyumba alikutwa akiwa na simu kinyume na kifungu namba 86,
kifungu kidogo cha kwanza na pili cha Sheria ya Magereza iliyofanyiwa
warekebisho mwaka 2002.
Baada ya ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa
upande wa mashtaka, mahakama iliupitia na kumwona Liyumba ana kesi ya
kujibu dhidi ya shtaka hilo linalomkabili, hivyo kumtaka ajitetee.
Liyumba alijitetea na kuomba mahakama kumfutia shtaka hilo na imuachie huru, kwa sababu kesi hiyo ilipangwa kumkomoa.
Alisisitiza kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya
kumkomoa, wakati akitumikia kifungo cha miaka miwili jela, yeye hajawahi
kuvunja sheria, kupewa adhabu wala kuonywa kwa kosa lolote.
Liyumba alidai simu inayodaiwa kuwa alikamatwa
nayo wakati akitumikia kifungo cha miaka miwili yenye namba 0653 004662
haifahamu na kwamba, ameiona mahakamani hapo. Aliongeza kuwa namba hiyo
lazima itakuwa imesajiliwa, hivyo mhusika halisi akitafutwa atajulikana.
Alidai Julai 2011, yeye alikuwa ni mfungwa
akitumikia kifungo cha miaka miwili na kwamba, unapofikishwa gerezani
lazima upekuliwe mara tatu na unavuliwa nguo zote za kiraia na kila kitu
chako kinahifadhiwa sehemu ambayo huwezi kuijua. Alidai kutokana na
ulinzi uliopo gerezani na selo aliyokuwapo, haoni jinsi ya mfungwa ama
mahabusu anaweza kuingiza simu
MWANANCHI
MWANANCHI


Post a Comment