Rais wa Marekani, Barack Obama
********
Rais Wa Marekani Barrack Obama amekiagiza kitengo cha ujasusi nchini
humo kusitisha ukusanyaji wa habari kutoka kwa simu za mamilioni ya raia
nchini humo na hata katika mataifa ya kigeni.
Akizungumza mjini Washington Obama pia amewaahidi viongozi wa nchi
washirika wa Marekani kwamba taifa lake halitachunguza mawasiliano yao
ya faragha hadi itakapolazimika kufanya hivyo kutokana na maswala ya
ki-usalama.
Tangazo hilo linajiri wakati ambapo kuna hasira ya kimataifa kuhusiana
na kiwango cha upelelezi unaofanywa na Marekani kufuatia ufichuzi wa
siri za kitengo hicho uliofanywa na aliyekuwa mchambuzi wa maswala
kijasusi nchini humo Edward Snowden.
Mwandishi wa BBC mjini Washington amesema kuwa makundi ya wanaharakati
watashangazwa na hatua ya kitengo hicho kuendelea kumiliki habari nyingi
za simu walizokusanya na kwamba haijulikana watazifanyia nini habari
hizo.
Hadhi ya kitengo cha ujasusi nchini marekani imeshushwa na ufichuzi wa bwana Snowden.
Wakati huohuo hotuba ya rais Obama kuhusu mabadiliko ya mpango wa upelelezi wa marekani yamepongezwa nchini Ujerumani.
Uhusiano kati ya Berlin na Washington uliwekwa katika mizani mwaka
uliopita baada ya kubainika kwamba marekani ilidukua simu ya chansela wa
Ujerumani Angela Merkel.a
Post a Comment