Bw Komeni
CHAMA cha demokrasia
na maendeleo (CHADEMA)
kimeendelea kutupiwa lawama
baada ya kada
mwingine wa chama
hicho bwana Abduli Komeni kuibuka
na kudai kuwa
chama hicho kimekuwa
kikiwatenga walemavu
,
Bwana Komei aliyasema
hayo baada ya
yeye kutopewa nafasi
ya kugombea ubunge
mwaka 2010 katika
jimbo la temeke
kupitia chama hicho.
Akizungumza na waandishi
wa habari Komeni
alisema kuwa kwa
yeye kunyimwa nafasi
hiyo jambo hilo
linapelekea kudhohofisha jitihada
za kuwatetea watu
wa kundi lake
yaani (Albino) kutoka
na kundi hilo
kuwa na uwakilishi
mdogo bungeni.
Aidha bwana Komeni
alisema kuwa watanzania
wasione Zitto kabwea
analalamika saizi wajue
kuwa hayo matatizo
hayajaanza leo katika
chama hicho,kwani hata
yeye hayo mambo
alifanyiwa lakini alipotaka
kuzungumzia mambo hayo
hakuweza kupata nafasi
kutokana na waandishi
kukataa kuandika habari
zake na hivyo
yeye kubaki akipata
tabu .
Pamoja na hayo
aliongeza kuwa kwasasa
anachosubiri ni kwenda
kuwasilisha barua yake
juu ya malalamiko
hayo kwa chama
cha maalbino ili
kukiomba chama hicho
kukaa na msajili
wa vyama vya
siasa nchini pamoja
na viongozi wa
chadema .
Na alipoulizwa na
waandishi wa habari
juu ya kuhama
kwenye chama hicho
kutokana na kuonekana
yeye kutojaliwa ,
Komeni alisema kuwa
swala hilo atalizungumza baadaye
na si swala
la haraka kiasi
hicho.
NA KENETH JOHN WA MATUKIODAIMA.COM ,DAR ES SALAAM
1 comments:
itz dangerous naona kila blog sasa hivi zinaandika baya la chadema.inamaana mazuri hayapo kabisaaa wanayofanya.poleni ila siri ya wamiliki wa blogs itajulikana maana zamani mlikuwa hamuandiki hayo mabaya japo yalikuwepo. ila leio mabaya ya chadema ndo habari kuu hata vyama vingine pia kuna maovu mengi xana. #BAHASHA YA KAKI#
ReplyPost a Comment