
Mwenyekiti
wa CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kikao cha siku moja cha
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo mjini
Zanzibar ,pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeipongeza Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, na wananchi wake kwa kuadhimisha miaka 50 ya
Mapinduzi.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Zanzibar,Rais Dkt. Ali Mohamed Shein na upande wa kulia ni Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara,Mh. Phillip Mangula pamoja na Katibu Mkuu wa CCM
Taifa,Mh. Abdulrahman Kinana.
*******
Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekuwa na kikao cha siku moja leo
tarehe 13/01/2014 mjini Zanzibar chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Taifa
wa CCM Dr. Jakaya Kikwete.
Pamoja
na mambo mengine Kamati Kuu imeipongeza sana Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, wazanzibari na watanzania kwa ujumla kwa kuadhimisha miaka 50
ya Mapinduzi ya Zanzibar. Aidha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imepongezwa kwa maandalizi mazuri na ya kufana ya sherehe hizo.
Kamati
Kuu imetambua na kupongeza hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa tangu
mapinduzi mwaka 1964 mpaka leo. Wito umetolewa kuyalinda na kuyaendeleza
mema yote yatokanayo na mapinduzi hayo na mafanikio yaliyoletwa na
serikali inayoongozwa na CCM.
Aidha Kamati Kuu imemteua Ndg. Mahmoud Thabit Kombo kuwa mgombea wa uwakilishi jimbo la Kiembesamaki kupitia CCM.
Kesho
mgombea huyu wa CCM atachukua fomu za tume za kugombea. Uzinduzi wa
kampeni za CCM utafanyika tarehe 22/01/2014 kwenye viwanja vya
Kiembesamaki ambapo mgeni rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Mohamed Gharib Bilal.
Kampeni
za CCM zitafungwa tarehe 01/02/2014 huko Chukwani na mgeni Rasmi
atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Ndg.
Balozi Seif Ali Idi.
Kampeni
itaendeshwa na Kamati ya Siasa ya wilaya ya Dimani viongozi na
wanachama wa wilaya husika, na ngazi zingine za Chama zitashirikiana na
ngazi ya wilaya kuhakikisha CCM inashinda tena jimbo hili.
Kamati
Kuu inawatakia kila lakheri kwenye kampeni na hatimaye uchaguzi huo.
Kampeni na hata upigaji kura uendeshwe kwa amani na utulivu kama ulivyo
utamaduni wetu.
Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
13/01/2014


Post a Comment