Balozi wa
Tanzania Nchini Oman Balozi Ali Ahmeid Saleh , akiongoza Ujumbe wa
Wafanyabiashara wa Oman, wakiwa na Kiongozi wao Rais wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara ya Oman (OCCI) wakiwasili katika bandari ya Zanzibar
wakitokea Dar-es-Salaam, kwa ziara ya siku tatu kuonana na
Wafanyabiashara wa Jumuiya ya Wafanyabiashara ya Zanzibar kuimarisha
Umoja wao ulioundwa hivi karibuni baina ya Oman na Tanzania.
Wafanyabiashara
wa Oman wakipokelewa Balozi wa Mdogo wa Oman Zanzibar na Wenyeji wao
Viongozi wa Jumuiya ya Wafayabiashara wa Zanzibar, wakiwasili kwa Boti
ya Kampuni ya Azam Kilimanjari 4.
Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Zanzibar wakiwapokea Wageni wao katika Bandari ya Zanzibar.
Balozi
Mdogo wa Oman Zanzibar Balozi Khalid Khamis na Rais wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara wa Oman Khalil Bin Abdallah Al Khonji wakiwasili katika
bandari ya Zanzibar kwaziara ya siku tatu..
Balozi wa Oman Nchini Tanzania Balozi Ali Ahmeid Saleh, akiongoza Ujumbe wa Wafanyabiashara wa Oman Zanzibar.
Balozi wa
Tanzania Nchini Oman Balozi Ali Ahmeid Saleh, akizungumza na Waandishi
wa habari ujio wa Ujumbe wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Oman Zanzibar
ili kukuza uhusiano wao wa makubaliano ya kuunda Jumuiya ya Pamoja ya
Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania.
Rais wa
Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Oman Bwa. Khalil Bin Abdullah Al Khonji,
akizungumza na waandhishi wa habari baada ya kuwasili katika bandari ya
Zanzibar kwa mazungumzo na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Zanzibar na
kuimarisha uhusiano wa Kibiashara kati ya Zanzibar na Oman
Wafanyabiashara
wa Oman wakimalizia kujaza fomu za Uhamiaji baada ya kuwasili Zanzibar
wakitokea Dar-es-Salaam, wakiwa Zanzibar watakuwa na Mkutano na Jumuiya
ya Wafanyabiashara ya Zanzibar na Wafanyabiashara kuzungumzia kuimaridha
Jumuiya ya pamoja ya Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania
Ujumbe wa
Wafanyabiashara wa Oman wakitoka katika chumba cha VIP baada ya
kumaliza taratibu zote za kiserekali za kuingia nchini. baada ya
kuwasili na boti ya kampuni ya Azam Marine ya Kilimanjaro 4.
Post a Comment