MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji, aliibua cheleko ndani ya
Mkutano wa klabu hiyo, baada ya kumtaka Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa
klabu hiyo Ibrahim Akilimali kuacha kuzungumza ovyo ovyo katika vyombo
vya habari wakati Katiba ya klabu yao haimpi mamlaka. Manji aliyasema
hayo, katika Mkutano wa mwaka wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi
wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam, baada ya kujibu swali la
mwanachama Msham Wazir ambaye ni Mwenyekiti wa Tawi la Bunju lilohoji
kuwa, Wanachama hawatambui nani ni nanni ndani ya klabu kwa kuwa kila
mtu anajifanya msemaji huku akimtolea mfano Akilimali.
Baada
ya swali hilo, wanachama waliofurika katika ukumbi huo, walisimama na
kushangilia na kumfanya Makamu Mwenyekiti Clement Sanga aliyekuwa
akiongoza Mkutano huo kukabidhi rungu hilo kwa Manji baada ya yeye kutoa
ufafanuzi kuwa, Katiba ya Yanga hakuna kifungu kinachowapa mamlaka
wazee kuzungumza.
“Katiba
ya Yanga haiwatambui wazee kabisa, na mtu akinielewa vibaya sawa tu,
kwani hakuna sehemu ya katiba inazungumzia wazee, kwani Msemaji Mkuu
katika klabu ya Yanga ni Mwenyekiti, Ofisa habari na hata mimi
nazungumza endapo Mwenyekiti akiwa hayupo au ameniagiza,”alisema Sanga.
Aidha
baada ya Sanga kujibu hivyo, alimkabidhi Manji jukumu la kufafanua
suala hilo na kusema kuwa, Akilimali ni Mzee wake lakini anakuwa
mvunjifu wa katiba ya Yanga kwa kusema sema katika vyombo vya habari
mambo ambayo hayastaili kuzungumzwa.
“Akilimali
anaongea kupita kiasi katika vyombo vya habari, kwani wewe sio msemaji
wa klabu jamani, unavunja katiba ya Yanga, mambo ya nyumbani unaongea
tu, eti Kaseja kafanyaje, jamani acha kufanya hivyo,”alisema Manji huku
akiwaomba ridhaa wanachama waamue nini cha kumfanya Akilimali na
kuwafanya wanachama kushangilia mwanzo mwisho.
Baada
ya kusema hayo, Manji alinyanyuka katika kiti alichokuwa amekaa na
kumfuata Akilimali na kuanza kuzungumza naye, huku wanachama
wakishangilia na wengine kuzomea kitendo hicho.
Akizungumzia
sakata hilo, Akilimali alikiri kukiuka katiba ya Yanga, na kusema kuwa,
anahisi alipandwa na wazimu bila kujijua na ndio sababu ya kuongea
katika vyombo vya habari bila idhini ya uongozi wake.
“Mimi
kusema kweli sina kinyongo kabisa, na uongozi wangu, wamenizuia
nisiongee katika vyombo vya habari, basi nitafanya hivyo, naisi ni
wazimu tu na ushabiki ulinipanda, nawaheshimu na kuwasikiliza viongozi
wangu, kama wamenipa onyo sawa tu,”alisema.
Post a Comment