Wafuasi wa CCM kata ya Nduli wakiwa wamemnyanya juu juu aliyekuwa mgombea udiwani kata ya Nduli Bw Mtove baada ya matokeo kumpa ushindi wa kishindo leo
Wafuasi wa CCM Iringa wakimpongeza
kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga kwa kufanikisha chama
hicho kushinda uchaguzi mdogo kata ya Nduli kama alivyopata
kumuahidi mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa
(Chadema) katika mikutano yake kuwa safari ya kumng'oa ubunge 2015
itaanzia katika uchaguzi huo mdogo kata ya Nduli kuwa lazima Msigwa
atake atatoa na asipo taka atatoa jimbo la Iringa mjini
..........................................................................................................................................................
CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa
wa Iringa kimefanikiwa
kutetea kata zake zote tatu ambazo leo
wananchi wameshiriki kupiga kura
kuwachagua madiwani kufuatia
nafasi hiyo kuwa wazi baada ya madiwani wake kufariki dunia
huku chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kikishindwa vibaya katika
uchaguzi huo.
Mbunge wa jimbo la
Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) ambae alikuwepo
eneo la Nduli akifuatilia matokeo
ya uchaguzi huo pamoja na wafuasi
wa Chadema alilazimika kuondoka katika eneo hilo baada ya
kubaini kuwa hali ya ushindi kwa Chadema ni ndoto.
Huku wafuasia wa
CCM wakionekana kumpongeza
aliyekuwa mgombea wa CCM kata ya Nduli pamoja na kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga kuwa kazi
yake imeonyesha inaonyesha wazi safari yake ya kulitwaa jimbo la Iringa mjini .
Katika matokeo ambayo mtandao huu umeyapata
ni kama ifuatavyo kwa vituo
vyote tisa ambavyo
wananchi wa Nduli walipata
kuvitumia kupiga kura ,kituo cha
Mawasiliano CCM
(57),Chadema(28),Zahanati CCM( 114),
Chadema ( 47), Shule Nduli CCM(70)
Chadema(39), KIngonzile shule CCM(105) Chadema(82),Mibata CCM(48) Chadema(103),
MTalagala CCM(95),Chadema(54),Godauni
CCM(138 ,Chadema(52),Njiapanda CCM (75) Chadema (52),Msisina CCM (156 ) Chadema (31)
Katika Matokeo hayo
ambayo hadi sasa majira ya saa
12.50 bado msimamizi wa uchaguzi
kutangaza CCM inaongoza kwa kura 854 huku
Chadema wakifuatia kwa kura 487
Mbali ya matokeo hayo ya kata ya Nduli pia
CCM imeshinda kata ya Ibumi na Ukumbi zote za wilaya ya
Kilolo.
Wakati katika kata ya Njombe mjini
mgombea wa Chadema amepata kukibwaga vibaya chama cha Mapinduzi
(CCM) ambapo matokeo yanaonyesha mgombea wa CCM amepata kuongoza
kituo kimoja pekee kwa tofauti ya kura 2 huku vituo vyote Chadema
ikiibuka kidedea.
Post a Comment