Mbunge
wa Jimbo la Kitope Balozi Seif akikabidhi msaada wa Bati kwa ajili ya
kusaidia uwezekaji wa Jengo la Klabu ya Soka ya Timu ya Kombora iliyopo
Kitope.
Mwalimu
Mkuu wa Skuli ya Kirombero Mwalimu Juma Simai akipokea msaada wa vifaa
vya kupikia chai vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif
Ali Iddi kwa skuli zote za jimbo hilo.Hafla hiyo imefanyika katika uwanja wa michezo wa Kombora Kitope.
Mbunge
wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akizindua na kukagua kisima cha
maji safi kiliopo Kijiji cha Mgambo ambacho kimejengwa kutokana na
Mfuko wa Jimbo la Kitope.
Mbunge
wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi msaada wa Magodoro,
Juzuu na Mashaf Ustadhi wa Madrasat Qiyamu Islamia ya Mgambo Wilaya ya
Kaskazini Unguja,akitekeleza ahadi aliyoipa Madrasa hiyo.
Makamo
wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mbunge wa Kitope Balozi Seif. Ali Iddi,
akizungumza na Wanafunzi wa Madrasat Qiyamu Islamia ya Mgombo Unguja ili
kufanya bidii katika kusoma na ili kuja kuwa Walimu Bora wa baadae wa
Elimu ya Dini ya Kiislam,(Picha na Hassan Issa – OMPR)
Na Othman Ame OMPR.
Walimu
wa Madrasa wameaswa kujiepusha na tabia ya kuwafundisha watoto
ushabiki wa Kisiasa kwa kutumia mafundisho ya Dini jambo ambalo
linaweza kuleta matabaka na ni hatari kwa watoto hao katika maisha yao
ya baadaye.
Mbunge
wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati wa
hafla fupi ya Kukabidhi msaada wa Magodoro, Misahafu, Juzuu pamoja na
fedha taslimu kwa ajili ya ununuzi wa mpira wa kusambazia maji kwa
Madrasat Qiyamu Islamia hafla iliyofanyika katika uwanja wa Skuli ya
Mgambo Wilaya ya Kaskazini “ B “.
Balozi
Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema jamii
katika baadhi ya maeneo Nchini imekuwa ikikosa utulivu wa kimaisha na
hatimae kuingia katika mgongano baina ya jamii kutokana na baadhi ya
walimu kuendeleza hulka ya kushawishi wanafunzi wao kujihusisha na
masuala ya Kisiasa.
Alisema
wakati umefika kwa walimu hao kuhakikisha kwamba wanasimamia vyema
ufundishaji sahihi uliosisitizwa katika Qurani pamoja na maamrisho yote
yaliyomo ndani ya mfumo mzima wa Dini ya Kiislamu.
Aliwataka
waalimu na wananchi kuendelea kuwa na subra hasa wakati wanapoomba
nguvu za ziada za kupatiwa misaada katika miradi yao ya maendeleo na
hata ile ya Kidini.
Credit: Zanzinews
Post a Comment