Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akifungua rasmi mradi wa maji wa Kigugu
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, akizungumza na wananchi wa Mlali.
*******
. Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla leo ameendelea na ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kwa kutembelea miradi ya mji wa Mvomero na Mlali, Kata ya Mlali, Tarafa ya Mlali mkoani Morogoro.
Mhe. Makalla ameridhishwa na kiwango cha mradi wa maji wa mji wa Mvomero na mpango kazi wa mkandarasi anayetekeleza mradi huo
“Nakubaliana na mpango kazi wenu na ninaamini kuwa mpaka mwezi wa tano, mtakuwa mmekamilisha mradi huu na kukabidhi kazi kwa Serikali na wananchi wa jiji la Mvomero waanze kupata maji”, alisema Mhe. Makalla.
“Napenda kusisitiza mkandarasi aachane na siasa na kurudi mahali pa kazi na kuanza kazi mara moja na kama kuna mambo yoyote, tutakaa chini na kuzungumza wakati kazi ikiendelea. Kinachotakiwa ni mradi kukamilika kwa wakati na maji yapatikane”, aliongeza Naibu Waziri.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Maji, ameweza kuona hali ya utekelezaji na maendeleo ya miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali katika mkoa wa Morogoro huku akisisitiza atahakikisha lengo la Serikali kuwapa wananchi wake maji linatimia.
Post a Comment