Waziri wa
nchi ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala bora Kepteni Mstaafu George
Mkuchika ameziagiza Halmashauri na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) kutoa mafunzo ya jinsi ya kupambana na rushwa kwa
mabaraza ya madiwani nchini.
Akizungumza
kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Iringa kilichofanyika
kwenye ukumbi wa Siasa ni kilimo Mkuchika alisema mafunzo hayo
yanatakiwa yafike mpaka kiwango cha kata ili kuongeza chachu ya
mapambano ya rushwa nchini.
Alisema
mafunzo hayo yanatakiwa kufika mpaka kiwango cha madiwani kwa kuwa ndio
wao wanaoishi na wananchi na miradi mingi ya maendeleo inafanyika huko.
Mkuchika
alisema jukumu la kuzui na kupambana na rushwa siyo la serikali peke
yake bali ni la kila mwanajamii, taasisi za umma, taasisi binafsi,
jumuiya za kidini pamoja na washirika wengine wa maendeleo wa kimataifa.
Alisema
ni wazi kuwa rushwa ni kikwazo kikubwa katika cha uwepo wa utawala usio
bora katika nchi yoyote Duniani na dawa sahihi ya kudhibiti ni kila
mmoja kuzingatia maadili.
Aliongeza
kuwa hatua hiyo itaiwezesha serikali kutekeleza majukumu yake ipasavyo
na pia wananchi kupata huduma bora kwa wakati na kuwa na maendeleo
tarajiwa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii katika mkoa wa Iringa.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa alisema ni
vema mafunzo kama hayo yakafika mpaka kwa wananchi wa kawaida ambao ndio
waathirika wakuu wa tatizo la rushwa badala ya kuishia kwenye mikoa na
wilaya tu.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mwamwindi alisema mafunzo hayo ni
muhimu na kuwa Halmashauri yake kjwa kushirikiana na kamanda wa TAKUKURU
kwa kutumia bajeti yao finyu watafanya mafunzo hayo kwa madiwani.
Chanzo: Hakimu Mwafongo



Post a Comment