TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wakimataifa utakaojadili uzuiaji wa uhalifu unaotokana na matumizi ya njia ya mtandao, unatarajia kufayika Jijini Dar es Salaam, Machi 27 hadi 28 mwaka huu.
Mkutano huo unatokana na kuwa Tanzania ni miongoni mwa baadhi ya nchi zinazokabiliwa na changamoto za uhalifu huo kwa njia ya mtandao.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa mifumo ya usalama kwa njia ya mtandao kutoka kampuni ya Codesoft Solution Ltd, Jonah Kyathe alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa fedha na Uchumi, Saada Mkuya .
Kyathe alisema mkutano utalenga katika kuzijadili changamoto mbalimbali zinazosababisha uhalufu na mwishoni washiriki watashauri serikali itunge sheria itakayo saidia kuzuia wizi huo unaotokana na matumizi mabaya ya mtandao.
“Mkutano huo utawashirikisha wadau wandani na nje zaidi ya 500 wakitoka Taasisi za fedha, Sekta binafsi, Jeshi la polisi, kampuni za mawasiliano na wataalamu wa masuala ya ulinzi,”alisema Kyathe.
Kyathe alisema uwezo wa kuzuia uhalifu huo hapa nchini bado ni wa kiwango cha chini ikilinganishwa na nchi kama Kenya na Uganda hivyo mkutano huo utajadili kwa kina namna ya kudhibiti suala hilo.
Mchambuzi wa mifumo ya usalama kutoka Codesoft Solution Ltd, Erastus Kamau, alisema pamoja na kujadili masuala ya usalama kwenye mabenki na taasis za fedha bado anaamini uwepo wa sheria ya kudhibiti makosa ya uhalifu huo inahitajika haraka.
“Mpaka sasa hakunakampuni yoyote nchini inayojihusisha na masula ya kuzuia uhalifu kwa njia ya mtandao ndio maana tukaamua kuchukua hatua hii ya kufanya mkutano huu na wadau wa masuala ya usalama”alisema Kamau.
Post a Comment