Shehe
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akisoma dua kabla ya kikao hicho cha
Baraza la Vyama Vya Siasa vyenye usajili kuanza katika ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaa
Sehemu
ya viongozi wa vyama vya siasa wakiomba dua katika kikao hicho cha
Baraza la Vyama Vya Siasa vyenye usajili kabla ya kuanza katika ukumbi
wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa katika kikao hicho cha Baraza la
Vyama Vya Siasa vyenye usajili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa
wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa katika kikao hicho cha Baraza la
Vyama Vya Siasa vyenye usajili kuanza katika ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa katika kikao hicho cha Baraza la
Vyama Vya Siasa vyenye usajili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya siasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha APPT-Maendeleo, Mhe Peter Mziray akisoma
hotuba yake katika kikao hicho cha Baraza la Vyama Vya Siasa vyenye
usajili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala toka kwa Mwenyekiti wa Barza la Vyama vya Siasa Mhe. Peter Mziray
Viongozin wakisikiliza hotuba kwa makini
Viongozi wa vyama vya siasa wakiwa kikaoni hapo
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akiwa na Kamishna Isaya Mungulu Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai DCI wakiwa wageni waalikwa kikaoni hapo
Rais Kikwete akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho
Rais Kikwete akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho
Rais Kikwete akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho
Viongozi wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete
Rais Kikwete akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho
Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe na Katibu wake Mhe Wilbroad Slaa wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete kwa makini
Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe akifuatilia hotuba hiyo
Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
Viongozi wakimpigia makofi Rais Kikwete
Viongozi wakiangua kicheko
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akitoa neno la shukurani
Rais
Kikwete, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariffa
Hamad, Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi na viongozi wa
vyama na maafisa wa serikali wakitelemka ngazini baada ya kupata chakula
cha mcha pamoja
Rais Kikwete na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariffa Hamad wakiongea
Sehemu ya wajumbe wa kikao
Wajumbe wa kikao
Wajumbe kikaoni
Wajumbe kikaoni
Rais Kikwete akiendelea na hotuba
Wajumbe wakisikiliza kwa makini
Rais Kikwete akimalizia hotuba yake
Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
Pokea rasimu ya katiba mheshimiwa...
Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
Rais Kikwete akisalimiana na Mhe Tundu Lissu baada ya kufungua kikao
Rais
Kikwete, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika picha ya kumbukumbu
na wenyeviti wa vyama vya siasa baada ya ufunguzi wa kikao hicho
Rais Jakaya Kikwete akipongezwa na Mhe Freeman Mbowe kwa hotuba nzuri
Picha ya pamoja na viongozi wa vyama vya siasa
Picha ya pamoja na makatibu wakuu wa vyama vya siasa
Picha ya pamoja na wajumbe wa kikao
Picha ya pamoja na viongozi wa dini na wa vyama vya siasa pamoja na wageni waalikwa
Rais Kikwete akiongea na Mhe James Mapalala
Rais Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila
Mhe William Lukuvi akisalimiana na Mhe Wilbroad Slaa
Rais Kikwete, Maalim Seif Shariff Hamad, Jaji Francis Mutungi Mhe Peter Mziray na Mhe Freeman Mbowe wakitoka nje ya ukumbi
Rais Kikwete akiongea na viongozi baada ya kufungua kikao hicho
Rais Kikwete akiagana na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya siasa Mhe Peter Mziray na viongozi wengine.
*********
*********
HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE,
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KWENYE KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA,
UKUMBI WA MIKUTANO WA KIMATAIFA WA
MWALIMU NYERERE, TAREHE 6 FEBRUARI, 2014
DAR ES SALAAM
Ndugu Peter Mziray, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama
vya Siasa;
Ndugu Vuai Ali Vuai, Makamu Mwenyekiti wa Baraza
la Vyama vya Siasa;
Mheshimiwa Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama
vya Siasa;
Ndugu Wenyeviti wa Vyama vya Siasa;
Ndugu Wajumbe wa Baraza la Vyama Siasa;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Utangulizi
Nakushukuru
ndugu Peter Mziray, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa na viongozi wenzako
kwa kunishirikisha kwenye kikao hiki maalum cha Baraza na kwa maelezo mazuri ya
utangulizi. Tutayatafakari ya kufanyika yafanyike. Nawapongeza kwa uamuzi wenu wa busara wa kuzungumzia
nafasi ya vyama vya siasa katika Bunge Maalum la kutunga Katiba. Jambo hili ni muhimu
kwa uhai, maendeleo na ustawi wa nchi yetu na watu wake. Mmeonesha moyo wa uzalendo
na ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu
Tangu
Baraza hili la vyama vya siasa lizinduliwe mwezi Mei, 2010, nimekuwa
nikifuatilia kwa karibu shughuli zake na jinsi linavyofanya kazi. Kwa kweli nimeridhishwa na hatua mliyopiga. Ndiyo maana mliponiita sikusita kuja. Nawaahidi kuwa nitaendelea kufanya hivyo
katika siku zijazo ili mradi tu nafasi iwepo.
Serikali Kuimarisha Uwanja wa Siasa
Ndugu Wajumbe;
Mtakubaliana
nami kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kujenga na kuendeleza demokrasia
ya vyama vingi na ushindani wa kisiasa.
Kuwepo kwa vyama 21 vyenye usajili wa kudumu vilivyo huru kuendesha
shughuli zao na Baraza la Vyama vya Siasa ni kielelezo tosha cha ukweli huu. Wazo la kuwa na Baraza hili liliibuka wakati
wa mchakato wa kutatua mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar uliozuka baada ya
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000. Kamati ya
Pamoja ya Mwafaka iliyokuwa na wajumbe kutoka CCM na CUF iliundwa ili kutafuta
suluhu ya mgogoro ule. Mojawapo ya mambo
ambayo Kamati hiyo ilipendekeza ni kuundwa kwa chombo kitachowezesha viongozi
wa vyama vya siasa kukutana mara kwa mara kujadili masuala ya kisiasa ili
kuepusha migogoro ya kisiasa.
Baada ya
Baraza kuundwa, mwaka 2009, Serikali ikaona haja ya kupanua wigo wa ushiriki na
kukifanya chombo hiki kuendesha kazi zake kwa mujibu wa Sheria. Matokeo yake Wenyeviti wa vyama vyote vya
siasa wakajumuishwa kufuatia marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa yaliyofanyika
mwaka 2009. Baraza la Vyama vya Siasa
likatambulika kisheria na majukumu yake kuorodheshwa katika Sheria husika. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ikapewa
jukumu la kuratibu na kugharimia shughuli za Baraza la Vyama vya Siasa.
Mabibi na Mabwana;
Nimeamua
kueleza chimbuko la Baraza la Vyama vya Siasa, ili Wajumbe wa Baraza na watu
wote wanaonisikiliza wajue kwamba Baraza hili limetokeaje kuwepo na lina nafasi
gani katika jamii na siasa za Tanzania.
Ni chombo kilichotokana na mafunzo tuliyopata katika migogoro ya kisiasa
huko nyuma. Baraza hili ndicho chombo ambacho
kikitumiwa vizuri na vyama vya siasa matatizo na malalamiko yao na masuala
mengine ya kisiasa yana mahali pa kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi. Aidha, ni jukwaa linalotoa fursa kwa vyama
vya siasa kuzungumzia masuala mbalimbali yenye maslahi kwa taifa na kukubaliana
kuhusu nini vyama vyenyewe vifanye au vishauri yafanyike na mamlaka husika. Ushauri
unaotolewa unawasilishwa Serikalini kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
ambayo ndio Sekretarieti ya Baraza hili.
Hakuna
chombo kingine zaidi ya Baraza hili kinachowakutanisha viongozi wote wa kitaifa
wa vyama vya siasa kujadili masuala ya kisiasa yenye maslahi ya kitaifa. Kwa kuzingatia nafasi yake na majukumu ya
Baraza hili, nawasihi viongozi wenzangu hususan Wenyeviti wa vyama vya siasa tulipe
uzito na tulitumie ipasavyo. Nawaomba
tuwe tunashiriki kwa ukamilifu katika vikao na shughuli za Baraza. Natambua kwamba kwa vile Baraza linajumuisha
vyama vyote hata Mwenyekiti wa Chama kidogo anaweza kuongoza Baraza inaweza
kutokupendeza kwa vyama vikubwa. Si
jambo la ajabu wala si jambo baya ndiyo maana na faida ya demokrasia. Wale wanaotoka vyama vikubwa wasichukie, wakifanya
hivyo wanakiuka kanuni moja ya msingi ya uongozi nayo ni “kiongozi mzuri pia
huwa ni mfuasi mzuri”. Hata mdogo analo
la maana la kuwanufaisha wote wadogo na wakubwa. Naamini Baraza likitumika vizuri
litatunufaisha wote: vyama vyote, nchi yetu na wananchi wote.
Mimi na
Mheshimiwa Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi kwa nafasi zetu hatushiriki moja kwa moja katika mikutano ya Baraza
hili. Pamoja na hilo bado tunalitambua, tunalithamini
na tunayachukulia maamuzi ya Baraza hili kwa uzito unaostahili. Ndiyo maana Chama changu kimemteua kiongozi
mzito anayenifuata kwa madaraka yaani Makamu Mwenyekiti, ndugu Philip Mangula
kuwa Mjumbe wa Baraza. Kutoka Zanzibar tumemteua Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu
Vuai Ali Vuai.
Kwa kweli
ingependeza sana kama viongozi wa vyama vingine nao wangetoa uzito unaostahili
kwa Baraza hili. Natoa rai kwa viongozi
wakuu wa vyama vya siasa, hususan wenyeviti kwa wao wenyewe kuwa Wajumbe wa
Baraza hili adhimu ili kulipa uzito na hadhi stahiki. Baraza hili lilianzishwa kwa ajili yetu, kujadili
masuala ya kuimarisha na kuboresha uwanja wa siasa nchini na kuweka mazingira
na uwanja ulio huru na sawa. Kusudi la kutaka
wenyeviti wote wa kitaifa wa vyama vya siasa wawe wajumbe wa Baraza ni
kuhakikisha kuwa Baraza linakuwa na uwakilishi wa watu wenye mamlaka kamili
kufanya maamuzi kwa niaba ya vyama vyao.
Ni muhimu sote tuone hoja hiyo na kuitumia fursa inayotolewa na
Baraza. Napenda kuwahakikishia ndugu
wajumbe kuwa Serikali itaendelea kusikiliza na kuheshimu ushauri wa Baraza hili
kwani ni chombo muhimu sana kwa mustakabali wa ustawi wa siasa na maendeleo ya
nchi yetu.
Ndugu Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa;
Jambo
lingine muhimu tunaloendelea kufanya ni kuimarisha Ofisi ya Msajili wa Vyama
vya Siasa ili iweze kumudu vyema majukumu yake.
Mwaka jana (2013) niliidhinisha
muundo mpya wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wenye vitengo vingi kuliko ilivyokuwa
kabla ya hapo. Muundo mpya unaoongozwa na
watumishi wenye taaluma nyingine mbalimbali badala ya kutegemea wanasheria peke
yake. Changamoto zinaongezeka na mazingira
ya kufanya kazi yanabadilika, hivyo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa itafaidika
na kuwa na watumishi wa kada nyingine kama vile wa sosholojia, sayansi ya siasa
na kadhalika.
Ili
kuhakikisha ufanisi zaidi, Serikali imedhamiria kuongeza bajeti ya ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa katika mwaka ujao wa fedha. Bila ya kufanya hivyo tutakuwa hatukufanya
kitu cha maana. Ofisi haitaweza kutimiza
wajibu wake. Kwa kweli itakuwa ni kuwaonea
kuwadai wafanye zaidi.
Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Baraza la Vyama vya
Siasa;
Nimeelezwa
na Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa, jambo moja linaloikwaza ofisi yake ili waweze
kutimiza ipasavyo jukumu lao la kuwa mlezi wa vyama vya siasa nchini ni mfumo
wa Sheria ya Vyama vya Siasa. Nimeelezwa
kuwa Sheria hii imeweka adhabu moja tu ambayo ni kukifuta Chama kinachofanya
makosa yaliyoainishwa katika Sheria badala ya kutafuta taratibu za
kurekebisha. Kwa maoni yake Sheria
haitoi nafasi ya kutosha ya kuvilea vyama vikue, vikomae na vijiepushe na migogoro
ya kisiasa ndani ya vyama na ndani ya jamii.
Kwa sababu hiyo, inamfanya Msajili aonekane kuwa ni mtu wa kutoa vitisho
vya kufungia vyama. Kwa maoni yake hatuna
budi kuangalia sheria hiyo upya ili iweze kushughulikia changamoto hizo.
Naiona
hoja ya Msajili na nampongeza sana kwa kuliona jambo hilo. Leteni mapendekezo yenu tuyatazame ili hatua
zipasazo zichukuliwe. Pamoja na hayo
usisubiri sheria. Mlezi hutoa ushauri na
kusaidia kupata ufumbuzi wa mambo mbalimbali yanayowatatiza viongozi na
wanachama wa vyama vya siasa. Usisite
kututembelea mara kwa mara kuzungumza nasi na kutushauri unavyoona inafaa. Itasaidia sana wakati tunasubiri Sheria
kufanyiwa marekebisho. Nafurahi kwamba
kazi hiyo unaifanya. Tafadhali
endelea. Pia usisite kutuita wote au
mmoja mmoja unapoona inafaa kufanya hivyo.
Nimeambiwa
mchakato wa kupitia upya Sheria hiyo na ile ya Gharama za Uchaguzi umeanzishwa
na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Bila ya shaka marekebisho ya Sheria ya Vyama yatasaidia kuboresha
uratibu wa shughuli za kisiasa hapa nchini bila kuingilia uhuru wa vyama vya siasa.
Vilevile marekebisho ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi yatasaidia kuhakikisha
wananchi wetu wanachagua viongozi kwa kuzingatia uwezo wao, mwenendo na ubora
wa sera za vyama vyao na si uwezo wao wa kifedha. Nimefurahi na nimefarijika sana na hatua hiyo. Ongezeni kasi ya kukamilisha zoezi hilo.
Ndugu Washiriki;
Naomba
kurudia tena kusema kuwa tunafanya hayo yote ili kuimarisha demokrasia ya vyama
vingi na ushindani wa kisiasa nchini.
Kwetu sisi Serikalini, vyama vya siasa ni wadau muhimu wa maendeleo ya
nchi yetu na watu wake. Kwa maana hiyo
tunapenda vyama viwe na uwezo wa kutekeleza wajibu huo. Kinyume chake, yaani vyama vinaweza kugeuka
na kuwa wakala wa kurudisha nyuma maendeleo.
Hii haikubaliki, itashangaza na kusikitisha.
Mada ya Kikao
Ndugu Mwenyekiti;
Kama
wote mnavyofahamu, nchi yetu ipo katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya. Hatua inayofuatia sasa ni Bunge Maalum la
Katiba kukutana na kujadili Rasimu ya Pili na kuamua ipasavyo. Kazi ya uteuzi wa Wajumbe 201 wa kuungana na
Wabunge na Wawakilishi katika Bunge hilo imekamilika na kesho watatangazwa. Ilikuwa
kazi ngumu sana. Watu wengi wazuri
walipendekezwa hivyo hujui umchague nani na umuache nani. Kwa vile hatuwezi kuwapeleka wote basi
tumewateua hao 201 na kuwaacha maelfu ya watu wazuri. Kama wote wanaofaa wangechukuliwa nchi
ingenufaika sana. Lakini hatuwezi kuwa
na Bunge la watu 5,000 hata China haifanyi hivyo. Ilikuwa hapana budi kuchagua baadhi yao
tu. Kwa ajili hiyo nawasihi wale wote wasioteuliwa
wasisononeke. Hawajapungukiwa sifa ila
nafasi hazitoshi.
Ndugu Wajumbe;
Wiki iliyopita nilitembelea ukumbi wa Bunge
Dodoma na kujionea mwenyewe maandalizi ya Ukumbi na vifaa unavyoendelea. Mambo yanakwenda vizuri. Nimeelezwa kuwa ifikapo tarehe 10 Februari,
2014 kila kitu kitakuwa tayari na majaribio kufanywa ya vifaa
vilivyofungwa. Nimeona tujipe wiki moja
baada ya hapo ili tuweze kurekebisha panapostahili. Kwa ajili hiyo nimekubaliana na Rais wa
Zanzibar niangalie uwezekano wa kuliitisha Bunge Maalum tarehe 18 Februari,
2014. Tutaitangaza rasmi siku hiyo
kupitia gazeti la Serikali.
Bunge la
Katiba ndilo lenye mamlaka ya kutunga Katiba mpya ya nchi yetu. Hatua zote zilizopita ni za kutoa
mapendekezo jukumu ambalo Tume ya
Mabadiliko ya Katiba imelikamilisha vyema.
Ipo Rasimu ya Katiba itakayofikishwa kwenye Bunge Maalum kujadiliwa na
kufanyiwa uamuzi. Ingekuwa Bunge la
kawaida au Baraza la Wawakilishi, Rasimu ya Katiba ndiyo Muswada wa Sheria
utakaofikishwa Bungeni na kwenye Baraza.
Wajumbe wa
Bunge hilo watambue kuwa wana dhamana isiyokuwa na mfano wake kwa nchi yetu na
Watanzania wenzao kwa jumla. Wanalo
jukumu la kuwapatia Katiba nzuri itakayodumu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo. Katiba itakayoimarisha Muungano badala ya
kuudhoofisha. Katiba itakayodumisha umoja,
amani na utulivu nchini badala ya kuvuruga.
Vilevile Katiba itakayoweka mazingira mazuri ya kisiasa, kijamii na
kiuchumi na kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi yetu na ustawi wa watu wake kwa
miaka mingi ijayo. Ili haya yafanyike ni
vyema Wajumbe wajue vyema kinachopendekezwa, wapambanue kinachofaa na
kisichofaa, na kubwa zaidi, watangulize maslahi ya taifa mbele kuliko maslahi
yao binafsi au ya makundi yao.
Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Baraza la Vyama vya
Siasa;
Mabibi na Mabwana;
Vyama
vya siasa vina nafasi ya pekee katika majadiliano ya Bunge Maalum la Katiba na
katika mchakato mzima wa kutunga Katiba mpya.
Mafanikio ya mchakato huu yatategemea sana kauli, mwenendo na matendo ya
vyama vya siasa. Ukweli ni kwamba vitendo
na kauli za viongozi, wanachama na wafuasi wa vyama vya siasa ndivyo
vitakavyojenga au kubomoa, na ndivyo vitakavyowezesha au kukwamisha mchakato huu.
Mimi
nataka vyama vijenge na kuwezesha mchakato ufanikiwe na Katiba mpya ipatikane
kwa wakati tunaoutarajia sote. Yaani
tufanye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2015 tukiwa na Katiba
Mpya. Mimi naamini kwa dhati ya moyo
wangu kuwa vyama vya siasa vikiamua Katiba ipatikane, itapatikana. Hivyo basi, kama vyama vya siasa vitaamua kishirikiana
kwa dhati, na kwa nia njema tutapata Katiba mpya bila kelele wala
mikwaruzo. Kama vyama vya siasa vitatambua
kuwa tunatengeneza jambo la kutunufaisha wote, yaani nchi yetu na watu wake na
siyo maslahi binafsi ya vyama vyao itakuwa hatua kubwa ya mwanzo ya kufanya
kazi ya Bunge kuwa rahisi. Pia kama
vyama vitakubali kuongozwa kwa nguvu ya hoja alizotoa Mjumbe na siyo Mjumbe
anatokea Chama gani au kundi gani, tutapata Katiba yenye maslahi kwa taifa letu.
Tutapata Katiba itakayoridhiwa na wananchi bila ya taabu.
Ninaposema
hayo sina maana kuwa vyama vya siasa au Wajumbe wanaotokana na vyama wasiende Bungeni
na maoni yao au na misimamo ya vyama vyao. La hasha! Nikifiria hivyo sitakuwa mkweli kwangu
mwenyewe. Nitakuwa najidanganya. Ninachosema ni kwamba, pamoja na kuwa na
maoni, mwongozo na misimamo ya vyama vyenu, lazima muwe na unyumbufu wa mawazo
kwa kiasi fulani ili mpate nafasi ya kusikiliza hoja za wengine zinazotofautiana
na zenu, kuzivumilia na kuzikubali pale ambapo kuna mantiki. Kwa lugha ya Kiingereza natoa wito wa “flexibility”. Muungwana hukubali mawazo
bora na yenye ukweli ya watu wengine. Hata wengine nao wanaweza kuwa na mawazo
bora kuliko yako. Muungwana ni yule anaekiri
ukweli huo na yuko tayari kupokea mawazo bora ya watu wengine hata kama watu
hao hawapendi. Kama tutakwenda kwenye
Bunge na azimio la kupinga kila wazo litakalosemwa na mtu fulani, hatutafikia
kupata Katiba mpya. Haitawezekana.
Ndugu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa;
Ndugu Wajumbe;
Mtakubaliana
nami kuwa Baraza hili na hasa ninyi viongozi mliokusanyika hapa leo mnayo
dhamana na jukumu la kipekee la kuipatia nchi yetu Katiba nzuri yenye maslahi
kwa nchi yetu na inayojali maslahi ya watu na kukubalika na watu wote. Katiba ambayo itakapotangazwa watu waseme
naam, hii ni Katiba inayojali maslahi ya nchi zetu mbili zilizoungana na kuwa
nchi moja miaka 50 iliyopita. Katiba
inayojali maslahi ya raia wa Tanzania ndani ya Muungano na ule upande wa
Muungano anakoishi au unakotoka kwa asili yake au historia yake.
Ni kwa
kutambua umuhimu huu wa vyama vya siasa ndiyo maana nilitoa wito kwa vyama vya
siasa kukutana na kuzungumza miongoni mwenu.
Ningependa mzungumze kuhusu namna bora ya kujadili rasimu ili mwishowe
tupate Katiba nzuri. Ningependa
mzungumze jinsi vyama vya siasa vitakavyoshirikiana hasa kutafuta ufumbuzi
wakati majadiliano yanapokuwa magumu kwa baadhi ya mambo.
Si vyema
mkadhani jawabu ni kushindana mpaka mwenye nguvu ashinde. Mnaweza kushindwa wote. Na mkishindwa, mjue sote tumeshindwa na nchi
imekwama. Msikubali kuifikisha nchi
hapo. Tuzidi kumuomba Mola atusaidie
tusifike hapo. Lakini, Mwenyezi Mungu
husaidia wanaojisaidia. Na sisi
tutengeneze namna bora ya kujisaidia ili Mungu akitia mkono wake mambo
yanajipa. Lililoonekana kuwa zito
linakuwa jepesi kama kanda la usufi.
Ndugu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa;
Nawaamini
nyote mliopo hapa mnaweza kutengeneza mfumo huo na taratibu hizo. Sina majibu wala maelekezo ya mfumo huo ni
upi. Nimekuja kutoa rai. Nimekuja kutoa maombi. Majibu mnayo ninyi. Mimi nasubiri jibu jema kama wanavyosubiri
Watanzania wengine. Nawaomba myatafakari
ninayosema na myape uzito unaostahili.
Mwisho
Narudia kuwashukuru
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa na Msajili wa Vyama vya Siasa, kwa
kunialika kuja kuongea na viongozi wa vyama vya siasa kupitia Baraza hili. Ni
matumaini yangu kuwa, miaka ishirini na mbili tangu mfumo wa vyama vingi
uanzishwe tena hapa nchini kwetu mwaka 1992, vyama vya siasa vimekomaa na vinaelewa
nafasi na umuhimu wake katika jamii. Hivyo basi, tutegemee matokeo mema katika
mkutano wenu huu wa kihistoria na mchakato utakaozaa matunda mema katika Bunge Maalum
la Katiba.
Kabla ya
kumaliza napenda kurudia kuwahakikishia kuwa mimi na Serikali ninayoiongoza tutaendeleza
ushirikiano wetu na Baraza. Tuko tayari kuitikia
wito wa kuja kuongea nanyi wakati wowote.
Baada ya kuyasema maneno yangu mengi, nawatakia kila heri katika Mkutano
wenu.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Ahsanteni kwa
kunisikiliza.








































































Post a Comment