
Tayari wanachama tisa wa chama hicho wamekwishachukua fomu kuonesha nia yao ya kuingia katika kinyang'anyiro hicho. Wanachama hao ni Hafsa Mtasiwa, Jackson Kiswaga, Godfrey Mgimwa, Edward Mtakimwa na Thomas Mwakoka.
Wengine ni Gabriel Kalinga, Msafiri Pamagil, Peter Mtisi na Grayson Kibasa.
Chama hicho kitaendesha kura ya maoni siku ya Jumamosi tarehe 8 Februari. Kura hiyo ni kwa ajili kupata jina la mgombea mmoja litakalowasilishwa kwenye Tume ya Uchaguzi. Tume ya Uchaguzi bado haijatangaza rasmi tarehe ya uchaguzi jimboni humo.


Post a Comment