Kocha
mkuu wa Wekundu wa Msimbazi Simba Zdracko Logarusic amefikia
makubaliano ya kuongeza mkataba na klabu hiyo utakaoendelea kumuweka
Msimbazi kwa miaka mingine miwili.
Katika makubaliano hayo Logarusic atalipiwa nyumba maeneo ya
Masaki,gari ya kutembelea,mafuta na posho ya kila siku huku pia mshahara
wake ukipandishwa kufikia Zaidi ya dola elfu 5.
Pia Logarusic amepewa jukumu la kuleta kocha wa viungo ili kuwajenga
wachezaji wa kikosi hicho katika harakati za kukiimarisha kikosi cha
Wekundu hao.
Logarusic amekubali kuitumikia Simba huku klabu kutoka nchi mbalimbali zikimmezea mate ili kumnasa kwenye vikosi vyao.
Tayari GOR MAHIA wamegonga hodi kuhitaji huduma ya kocha huyo
aliyewahi kuifundisha timu hiyo ya nchini Kenya ambayo kwasasa haina
matokeo mazuri sana.
Mbali ya Gor Mahia klabu mbili za nchini GHANA na klabu moja ya MISRI
nazo zinaendelea kufuatilia nyendo zake ikiwa pamoja na kumshawishi
aachane na Simba na wako tayari kutoa dau nono.
Wakati huo huo kocha msaidizi wa klabu hiyo Suleiman Matola naye
atafaidika kutokana na kuongezewa maslahi katika mkataba wake atakaopewa
baada ya kuonekana ana ushirikiano mzuri na Logarusic baada ya kocha
huyo kumpigia upatu wa kutaka kuendelea kubaki naye kama msaidizi wake.
SOURCE: SuperMario Blog



Post a Comment