Michuano
 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea Leo (Machi 19 mwaka huu) kwa 
mechi kati ya Yanga na Azam itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
 kuanzia saa 10.30 jioni.
Tiketi
 kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa saa 2 asubuhi katika magari 
maalumu kwenye vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Ubungo 
Terminal, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Samora/Ohio, OilCom Ubungo, 
Buguruni Shell, Dar Live- Mbagala, kituo cha daladala Mwenge na Uwanja 
wa Taifa.
Baada
 ya saa 6 mchana mauzo yote yatahamia Uwanja wa Taifa ambapo milango kwa
 ajili ya mechi itakuwa wazi kuanzia saa 7.30 mchana.
Viingilio
 katika mechi hiyo vitakuwa sh. 30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B 
na C wakati viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani kiingilio ni sh. 
7,000.
Mechi
 hiyo itachezeshwa na mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam ambapo 
atasaidiwa na Anold Bugado (Singida), Florentina Zablon (Dodoma) na Lulu
 Mushi (Dar es Salaam). Kamishna wa mechi hiyo Emmanuel Kavenga kutoka 
Mbeya wakati mtathimini wa waamuzi ni Alfred Rwiza wa Mwanza.


Post a Comment