WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia leo amemwakilisha waziri mkuu Mizengo Pinda katika mazishi ya aliyekuwa mkuu
wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Marehemu Moshi Chang'a.
Katika mazishi hayo yalihudhuriwa na mamia ya
wakazi wa Manispaa ya Iringa na viongozi wa serikali kutoka mikoa
mikoa mbali mbali nchini pia spika wa bunge Anne Makinda alitumia
nafasi hiyo kuueleza umma siri nzito iliyofichika dhidi yake ya
marehemu Chang'a mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza
ulioshirikisha vyama vingi kuwa bila marehemu huyo asingeweza kuwa
mbunge kutokana na kubanwa na chama cha upinzani cha NCCR Mageuzi kwa
kipindi hicho
"Mimi
nimekuwa kwa niaba yangu mwenyewe na jimbo la Njombe kusini ambalo
mimi ni mbunge wake ....mwaka 1995 marehemu alikuwa ni katibu wa CCM
Njombe na ndio mwaka ambao mfumo wa vyama vingi ulianza na yeye
ndie alikuwa katibu na jimbo hilo upinzani ulilizingira
kweli na hata kwa kukanyanga mguu kulikuwa hakuna ila bila Chang'a
kweli jimbo hilo niseme ukweli lingekuwa limechukuliwa na Upinzani
na kwa kipindi hicho chama chenye nguvu zaidi kilikuwa ni NCCR Mageuzi "
Akizungumza
wakati wa kutoa salama mbali mbali kwa viongozi mjini Iringa Spika
Makinda alisema kuwa kwa mara ya kwanza mwaka 1995 alibanwa kupita
kiasi na NCCR Mageuzi katika jimbo lake la uchaguzi
la Njombe kusini na kuwa bila marehemu huyo ambae kwa kipindi hicho
alikuwa ni katibu wa CCM wilaya ya Njombe kamwe asingeweza kuwa mbunge .
Mkuu
wa mkoa wa Rukwa injinia Stella Manyanya alisema kuwa mkoa wake
amempoteza kiongozi mzalendo na aliyependa kazi yake na kuwa hata
akiwa safarini hakuwa na shaka na utendaji kazi wa mkuu huyo wa
wilaya na kuwa siku zote mbali ya kuongoza kama kiongozi wa serikali
ila wakati mwingi alitumia
kuwahubiria upendo wananchi wa wilaya yake.
Kwani
alisema kuwa alikuwa hawezi kuanza mkutano bila kumhubiri mwenyezi
Mungu mbali ya kuwa yeye alikuwa muumini wa dini ya Kiislam ila alikuwa
akihubiria dini ya kikristo .
Hata
hivyo alisema kuwa hadi kesho anaamini alishinda ubunge jimbo
hilo mwaka 1995 si kwa uwezo wake bali alishinda kwa uwezo wa marehemu
Chang'a ambao alionyesha uwezo mkubwa wa kumnadi na hata kufanikiwa
kuwa mbunge wa jimbo hilo na leo kuwa spika wa bunge .
Alisema
iwapo angekwama kuwa mbunge mwaka 1995 basi yawezekana leo
asingekuwa spika kwani angekuwa amekata tamaa ama angekuwa mbunge
mwingine katika jimbo hilo.
Aidha
alisema mbali ya kushinda ubunge wake bado wapinzani walikwenda
mahakamani kupinga matokea ila Chang'a alisimama na makada wenzake
wawili moja akiwa ni marehemu sasa katika kumtetea mahakamani kwa
miaka minne yote na mbali ya hujuma kubwa zilizokuwa zikifanywa
na Halmashauri ya Njombe kwa kuharibu baadhi ya nyaraka za ushahidi
ili kuwawezesha NCCR Mageuzi kushinda kesi hiyo japo kwa Chang'a
walishindwa kutokana na kuwa na nyaraka hizo kwa mwenendo mzima wa
mchakato wa uchaguzi huo hadi mahakama ilipompatia ushindi yeye kama
mbunge halali wa jimbo hilo.
"
Leo nafanya kazi hii ya uspika kwa kuwa Chang'a ndie aliyeniweka hapa
na bila yeye kujituma mimi nisingesimama hapa kama spika ....jamani
nasema tuendelee kujituma katika
kazi zetu kama alivyofanya marehemu Chang'a nasema kila mmoja atapimwa
utendaji kazi wake hapa duniani "
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro akimuelezea
Chang'a wakati wa kutoa salam hizo alisema kuwa kamwe hata sahau
utendaji kazi wa mkuu huyo wa wilaya ambae amepata kufanya nae kazi
katika wilaya ya Makete ambapo yeye akiwa mkurugenzi Chang'a alikuwa ni
kiongozi wa CCM wilaya hiyo na baada ya kwenda
Mbeya pia Chang'a amefanya kazi kama mkuu wa wilaya katika mkoa huo
.
Kandoro
alisema kuwa utendaji kazi na utumishi uliotukuka wa Chang'a ni
mfano wa kuigwa kwa watumishi wengine wa umma katika Taifa hili.
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma alisema kuwa mkoa wa
Iringa umepata pigo kubwa kwa kifo cha mkuu huyo wa wilaya hasa
ukizingatia mchango mkubwa wa kimaendeleo ambao amepata kuonyesha ndani
ya mkoa na nje ya mkoa na kuwa kamwe mkoa utaenzi yote aliyoyaacha .
Mbunge
wa jimbo la Iringa mjini
mchungaji Peter Msigwa alisema kuwa wananchi wa Manispaa ya Iringa na
mkoa wa Iringa tumeendelea kupoteza wakuu wa wilaya na kuwa mbali
ya Chang'a pia tumepata kumpoteza mkuu wa wilaya ya Tabora na kuwa
viongozi hao wote ni pengo kubwa kwa Taifa .
Mbunge
Msigwa alisema kuwa akiwa kama mbunge wa jimbo hilo la Iringa mjini na
kiongozi wa Chadema wilaya hiyo amepokea kwa masikitiko kifo hicho na
kuwa sote kama viongozi tunapaswa kuangalia ni barua gani ambayo
inaachwa kwa jamii baada ya kuondoka na kuwa Chang'a alikuwa ni
kiongozi asiyependa kumchukia mtu na kila wakati alikuwa ni mtu wa
kucheka na kila mmoja.
Awali
akiwasilisha salama za serikali waziri Ghasia alisema kuwa kifo
hicho kimeacha pengo kubwa na kumtaja marehemu Chang'a katika mkuu wa
wilaya wa mfano ambae hakupenda kukataa wala kuonyesha kupinga kwa
sehemu yeyote anayopangiwa kwenda kuwakilisha wananchi .
Viongozi
wengine waliopata kushiriki katika mazishi hayo ni pamoja na
viongozi msaidizi wa Rais Jakaya Kikwete katika masuala ya siasa Ikulu
Rajab Luhwavi pia viongozi
kutoka mkoa wa Mwanza , Singida ,wabunge wa bunge la jamhuri ya
muungano akiwemo mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati na
Lediana Mafulu (CCM) naibu waziri wa maliasili na utalii Mahamudu
Mgimwa ambae pia ni mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazin,baadhi ya
wajumbe wa bunge la katiba kutoka
mkoa wa Iringa na wakuu wa wilaya mbali mbali akiwemo mkuu wa wilaya
ya Kibondo Venance Mwamwoto mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Letisia Warioba
,mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita na wengine wengi
Post a Comment