Mratibu
wa Chanjo Zanzibar Bw. Yusuf Haji Makame akizungumza na wandishi wa
Habari kuhusu wiki ya chanjo Afrika itayozinduliwa kesho na Waziri wa
Afya Mhe. Juma Duni Haji uzinduzi huo utafanyika kituo cha Afya Chumbuni
Mjini Zanzibar.
Mdhibiti
magonjwa - Kitengo cha Chanjo Wizara ya Afya Bw. Abdulhamid Ame akitoa
ufafanuzi kuhusu Chanjo wakati wa Mkuta na wandishi wa Habari.
Muandishi wa Habari wa Staa TV Abdallah Pandu akitaka ukiuliza swali kuhusu wiki ya Chanjo Afrika.
Baadhi
ya wandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mratibu wa
Chanjo Zanzibar Bw. Yusuf Haji (hayupo pichani) kuhusu siku ya Chanjo
Afrika katika ukumbi wa Mazsons Hotel Shangani Mjini Zanzibar.PICHA NA
MAKAME MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR.
Na Salum Vuai, MAELEZO
WAKATI
bara la Afrika linaanza wiki ya chanjo za kujikinga na maradhi kwa
watoto kesho (April 24), Waziri wa Afya Mhe. Juma Duni Haji, anatarajiwa
kuzindua wiki hiyo kwa upande wa Zanzibar.
Uzinduzi
huo ambao unafanyika Tanznaia nzima na katika nchi zote za bara la
Afrika, kwa Zanzibar umepangwa kufanyika kitaifa katika kituo cha afya
Chumbuni Wilaya ya Mjini.
Aidha
shughuli kama hiyo itafanyika katika wilaya zote kumi za Unguja na
Pemba, ambapo wakuu wa kila wilaya wanatarajiwa kuzindua katika ngazi
vituo mbalimbali vilivyomo katika wilaya zao, kuanzia leo Aprili 24 hadi
30, mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika hoteli ya Mazson iliyoko Shangani mjini
Unguja, mratibu wa chanjo Zanzibar Yussuf Haji Makame, alisema huduma
hizo zinatolewa kutokana na agizo la Shirika la Afya Ulimwenguni
(W.H.O), kwamba ifikapo wiki ya mwisho ya mwezi Aprili kila mwaka, nchi
zote za bara la Afrika zitoe huduma hizo kitaifa.
Alifahamisha
kuwa, zoezi hilo linawalenga watoto wote walio chini ya miaka miwili
ambao, ama hawakukamilisha chanjo au hawajapata kabisa katika awamu
iliyopita.Aidha,
alisema dhamira ya chanjo hizo ni kuwakinga watoto na maradhi
mbalimbali yanayoweza kuzuilika kwa chanjo ikiwemo polio, pepo punda
surua na mengineyo.
Afisa
huyo aliwataka wananchi wote wenye watoto wa umri huo na wengine walio
chini ya miaka mitano, kuwapeleka watoto wao vituoni na kuhakikisha
wanapata chanjo hiyo na kumaliza dozi ili kuwakinga na maradhi hayo, na
hivyo kuliwezesha taifa kuwa na kizazi chenye afya bora.Alisema
kazi hiyo itaanza katika vituo vyote mawilayani kuanzia saa 2:00
asubuhi hadi saa 10:00 jioni kwa siku zote saba.
Akitoa takwimu za hali ya maradhi ya surua kwa mujibu wa utafiti wa
W.H.O, Makame alisema mwaka 2011 vifo 158,000 vilivyosababishwa na
ugonjwa wa surua viliripotiwa.
Alisema
ripoti hiyo ilifafanua kuwa, kwa mujibu wa takwimu hizo, vifo 430
vilitokea kila siku, na kwamba kila baada ya saa moja kuliripotiwa vifo
18.Kwa
upande wake, Afisa Mdhibiti Magonjwa katika kitengo cha chanjo Zanzibar
Abdulhamid Ameir, alisema katika muongo wa chanjo barani Afrika
ulioanza mwaka 2011 ambao unatarajiwa kukamilika 2020, mikakati
madhubuti inahitajika kuhakikisha magonjwa yanawakumba watoto
yanatoweka kabisa.
Miongoni
mwa mikakati hiyo, ni kutoa dozi ya pili kwa chanjo ya kukinga surua
kuanzia mwezi ujao, tafauti na miaka iliyopita ambapo kulikuwa
kukitolewa dozi moja tu.Alisisitiza
kuwa, lengo la W.H.O. ni kuona ifikapo mwaka 2020 tatizo la maradhi ya
watoto yanamalizwa au kupunguzwa kwa asilimia kubwa.Alihitimisha
kwa kusema, huduma zinazozinduliwa leo, zinafanyika Tanzania nzima, na
akasisitiza wananchi wasipuuze kuwapeleka watoto wao ili kuwakinga na
maradhi hayo.
Post a Comment