Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ASHANTI, RHINO, JKT Oljoro RASMI ZAPOROMOKA DARAJA LA KWANZA


OLJORO
Rhino ya Tabora, Ashanti United na JKT Oljoro rasmi wameteremka daraja na kurejea Ligi Daraja la Kwanza.Ashanti imeshuka baada ya kuchapwa bao 1-0 na Prisons ya Mbeya katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, leo.

ASHANTI UNITED
Wachezaji wa Ashanti United, walilia kwa uchungu wakionyesha kutofurahia kuteremka daraja.
Rhino nao wakiwa nyumbani Tabora, leo wamepigwa mabao 2-0 na Ruvu Shooting. Hamis Mohammed na Elias Maguri ndiyo walioimaliza timu hiyo ya Tabora.
RHINO

Mjini Arusha, JKT OLjoro wameteremka rasmi baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar. Timu hiyo ya jeshi inakuwa timu ya tatu kuteremka daraja.

Kutokana na kuteremka kwa timu hizo, Ndanda FC, Stand ya Shinyanga na Polisi ya Morogoro ndiyo wamepanda rasmi Ligi Kuu Bara.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top