RASMI Azam fc wamefanikiwa kutwaa
ubingwa wa ligi kuu sokA Tanzania bara msimu wa 2013/2014 baada ya
kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City FC kwenye uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya.
Kwa matokoe hayo, Azam fc wamefikisha pointi 59 kileleni ambazo haziwezi kufikiwa na klabu yoyote ile, huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Kwa matokoe hayo, Azam fc wamefikisha pointi 59 kileleni ambazo haziwezi kufikiwa na klabu yoyote ile, huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Taarifa
kutoka Mbeya zinaeleza kuwa mechi iliingia dosari baada ya wachezaji wa
Mbeya City kumshambulia mwamuzi kutokana na kutoridhishwa na maamuzi
yake.
Mtandao huu unafuatilia kwa kina kujua nini kilichosababisha tafrani hizo na baadaye utapata taarifa rasmi.
Mbeya City baada ya kuchapwa leo hii, wanabakia katika nafasi ya tatu kwa pointi 47.
Rasmi
wameshajiengua kutafuta nafasi ya pili kwasababu hata kama watashinda
mechi yao ya mwisho dhidi ya Mgambo JKT aprili 19 watafikisha pointi 50
ambazo zimepitwa na Yanga.
Kwa mazingira hayo, Mbeya City wameshika nafasi ya tatu, Yanga ya pili na Azam fc ni mabingwa wapya.
Yanga
waliokuwa wanafukuziana na Azam fc kuwania ubingwa wameshinda mabao 2-1
dhidi ya JKT Oljoro katika dimba la Shk. Amri Abeid jijini Arusha,
lakini ushindi huo haujawasaidia chochote kutokana na ushindi wa Azam
fc
Na Baraka Mpenja wa fullshangwe, Dar Es Salaam
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA CHINI



Post a Comment